https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

/ 1 7 9

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

• Kuonyesha uhusiano kati ya jamii ya ufalme wa Kristo, Kanisa, na wajibu wake wa kuonyesha huruma na haki katika jamii ya ufalme, yaani, Kanisa kama mwili wa Kristo ulimwenguni limeitwa kutangaza Habari Njema kwa maskini, na jinsi ambavyo Kanisa limeitwa kuakisi maisha ya Enzi Ijayo kupitia matendo yake ya haki kwa niaba ya maskini. Pia kuonyesha kwamba, kupitia maisha na utume wa Kanisa, kwa uweza wa Roho Mtakatifu, Watu wa Mungu leo wanaonyesha na kufurahia shalom ile ile inayozungumzwa katika Agano la Kale. • Kuonyesha jinsi jamii hii mpya inavyoonyesha ukarimu mkubwa kwa wahitaji ndani ya jamii, hasa kwa wajane, yatima, na maskini katikati yetu, na vile vile kutoa misaada kwa makanisa mengine nyakati za majanga na matatizo. • Kuelezea namna ambavyo jamii hii mpya imeitwa kuwa mtetezi wa maskini, ambayo ni alama ya utume halisi wa Kikristo. Utetezi huu unajumuisha kutokuwa na ubaguzi au upendeleo kwa sababu ya matabaka au tofauti kati ya washirika wa mwili wa Kristo, kudhamiria kuishi kama jamii ya matendo mema kwa niaba ya maskini na walio hatarini, na kufanya kazi ili kusaidia kukidhi mahitaji halisi ya wanaoumizwa, hasa wale walio katika nyumba ya Mungu. • Kutambua maana ya Kanisa kama jamii mpya ya Ufalme kwa ajili ya utume wa mijini, ikiwa ni pamoja na hitaji la kutangaza Habari Njema kwa maskini (yaani, kuwaheshimu maskini kama watu ambao wamechaguliwa na Mungu, ambao Yesu alijihusisha nao, ambao hawatakiwi kudhalilishwa kamwe bali kuhudumiwa kwa haki na huruma kwa kutarajia mabadiliko yao na mchango wao kamili katika mchakato huo). • Kufanya muhtasari zaidi wa maana ya mtazamo huu, ikijumuisha kwamba Kanisa lazima litende kwa kuzingatia kwamba Mungu amewachagua maskini (yaani, kutetea maslahi yao, kudumisha haki zao, na kutoonyesha upendeleo katika mambo yetu katika Kanisa); tunapaswa kuwa wakarimu katika kukidhi mahitaji ya maskini, kugawana mali zetu, kuwafadhili wageni na wafungwa, na kuonyesha upendo kama tulivyoonyeshwa. • Kuelezea maana ya mwisho (na pengine muhimu zaidi) ambayo ni kwamba Kanisa lazima litafute haki na usawa katika kushughulika na maskini katikati yetu na katika ulimwengu; hatupaswi tu kukidhi mahitaji yao, bali pia kujitahidi kushughulika na mifumo na mahusiano kwa namna ambayo itasababisha utendaji wa haki zaidi. Kama vile Bwana katika Agano la Kale alivyodai kwamba jamii ya agano itoe rasilimali kwa maskini, vivyo

4

Made with FlippingBook Annual report maker