https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
1 8 0 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
hivyo Kanisa linapaswa “kuishi Injili ya mafanikio ya kweli,” kwa kutafuta haki na usawa kwa niaba ya maskini katika shughuli na masuala yote.
Niambie, Wewe Ndiwe?
Luka 7:18-23 – Wanafunzi wa Yohana wakamletea habari za hayo yote. 19 Ndipo Yohana alipowaita wawili katika wanafunzi wake, akawatuma kwa Yesu akiuliza, Wewe ndiwe yule ajaye, au tumtazamie mwingine? 20 Nao walipofika kwake, walisema, Yohana Mbatizaji ametutuma kwako, akisema, Wewe ndiwe yule ajaye, au tumtazamie mwingine? 21 Na saa ile ile aliwaponya wengi magonjwa yao, na misiba, na pepo wabaya; na vipofu wengi aliwakirimia kuona. 22 Ndipo alipojibu, akawaambia, Nendeni mkamweleze Yohana hayo mliyoyaona na kuyasikia; vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, maskini wanahubiriwa habari njema. 23 Naye heri mtu ye yote asiyechukizwa nami. Huduma ya Yesu kama Masihi ilianza katika eneo la Yudea kwa msisimko na matarajio makubwa, lakini haikuwa wazi mara moja kwa wote kwamba alikuwa Masihi, na hii ni kweli hata kwa Yohana Mbatizaji. Asili ya ajabu ya miujiza na matendo makuu ya Yesu ilizidi kupata hadhira katika siku za mwisho za Yohana Mbatizaji. Huduma ya Yohana ilivyopungua, ndivyo Yesu alivyoongezeka katika upeo na ushawishi (taz. Yoh. 3:30). Yohana alibatiza watu kwa ajili ya toba katika matazamio ya kufunuliwa kwa tangazo la Yesu la Ufalme wa Mungu, na Yesu alionyesha nguvu zake kupitia miujiza yake, mahubiri yake, na kupitia asili ya tabia na maisha yake mwenyewe. Kila sehemu ya asili na utu wa Yesu na kile alichofanya kilithibitilisha uhalali wa madai yake: Yesu wa Nazareti alikuwa Masihi wa Mungu, aliyetangaza kwamba Ufalme umekuja kupitia ujio wake duniani. Habari hii ya miujiza ya Yesu ilipokuwa ikienea katika Uyahudi wote na nchi za kandokando, wanafunzi wa Yohana walisikia matendo yake, wakaenda kumpasha Yohana habari. Yohana aliwatuma wawili miongoni mwa wanafunzi wake kwa Yesu na swali la moja kwa moja: “Wewe ndiwe yule ajaye, au tumtazamie mwingine?” Kulikuwa na ushahidi wa kutosha katika kazi na msimamo wa Yesu kuweza kufunua angalau wito wa kinabii juu ya maisha ya Mnazareti. Swali la Yohana halipaswi kutafsiriwa kama ushahidi wa kwamba alikuwa na mashaka au kwamba kulikuwa na hali yoyote ya kutokuelewana kati yao: swali lake linaonyesha hamu ya Yohana ya kufahamu ukweli kwa namna ya wazi zaidi, hasa katika maana ya ushuhuda wa Yesu mwenyewe kuhusu utambulisho wake. Luka anatuambia kwamba saa ileile ambayo Yesu alisikia swali kutoka kwa wanafunzi wa Yohana, alianza kuwaponya watu magonjwa na mateso yao mengi,
Ibada
4
Made with FlippingBook Annual report maker