https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

/ 1 8 1

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

na kutoa mapepo, na kuwapa vipofu kuona tena. Bila shaka Yesu alitoa uthibitisho mwingi kama nini kwa Yohana kuhusu utambulisho wake! Katika suala la idadi na utofauti, tunaweza kusema kwa urahisi kwamba Yesu aliwafanya wanafunzi wa Yohana waweze kusadiki kikamilifu kwamba Kristo alikuwa amebeba uweza wa Ufalme wa Mungu ndani yake, na kwamba Mungu alikuwa akifanya kazi kupitia yeye kuonyesha matendo ya ukombozi, uponyaji, na miujiza. Baada ya onyesho hili lenye nguvu la mamlaka na nguvu za Ufalme wake mwenyewe, Yesu aliwajibu wanafunzi wawili wa Yohana kwa kuwapa maelezo juu ya maana ya yale ambayo alikuwa ameyafanya. Yesu anawaagiza waende kumwambia Yohana mambo ambayo wao binafsi walimwona Yesu akifanya—wamwambie Yohana hasa kuhusu kazi ambazo walikuwa wamemshuhudia akizitenda. “Vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, maskini wanahubiriwa habari njema.” Na Yesu anamalizia kwa msemo wa ajabu sana kwamba asiyechukizwa naye amebarikiwa. Hapa tunapata kwa muhtasari maana ya wazi zaidi ya uthibitisho wa Yesu mwenyewe wa utambulisho wake. Yesu alijuaje kwamba Yohana angeelewa maana ya miujiza na uponyaji wake kuwa ishara ya umasihi wake? Kwa nini alikuwa na hakika kwamba kumwambia Yohana kwamba maskini wanahubiriwa Injili ya Ufalme kungekuwa uthibitisho usio na shaka kwamba yeye ndiye Masihi wa Mungu. Labda maandiko machache yanaweza kuonyesha kwa nini: Isa. 32:3-4 – Tena macho yao waonao hayatakuwa na kiwi, na masikio yao wasikiao yatasikiliza. 4 Tena moyo wa mtu mwenye hamaki utafahamu maarifa, na ndimi zao wenye kigugumizi zitakuwa tayari kunena sawasawa. Isa. 35:5-6 - Ndipo macho ya vipofu yatafumbuliwa, na masikio ya viziwi yatazibuliwa. 6 Ndipo mtu aliye kilema ataruka-ruka kama kulungu, na ulimi wake aliye bubu utaimba; maana katika nyika maji yatabubujika; na vijito jangwani. Isa. 42:6-7 - Mimi, Bwana, nimekuita katika haki, nami nitakushika mkono, na kukulinda, na kukutoa uwe agano la watu, na nuru ya mataifa; 7 kuyafunua macho ya vipofu, kuwatoa gerezani waliofungwa, kuwatoa wale walioketi gizani katika nyumba ya kufungwa. Isa. 42:16 – Nitawaleta vipofu kwa njia wasiyoijua; katika mapito wasiyoyajua nitawaongoza; nitafanya giza kuwa nuru mbele yao; na mahali palipopotoka kuwa pamenyoka. Haya nitayatenda, wala sitawaacha.

4

Made with FlippingBook Annual report maker