https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
1 8 2 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
Isa. 61:1-3 - Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao. 2 Kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao; 3 kuwaagizia hao waliao katika Sayuni, wapewe taji ya maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito; wapate kuitwa miti ya haki, iliyopandwa na Bwana, ili atukuzwe. Jibu la Yesu linaonyesha Masihi angekuwa mtu wa aina gani, na kwa nini kazi yake na matendo yake vinalingana kikamilifu na utambulisho huo wa Masihi. Uponyaji wa Yesu na kuhubiri Habari Njema kwa maskini ni ishara za enzi ya Kimasihi, kwamba Ufalme wa Mungu umekuja, na muhimu zaidi, kwamba Yesu wa Nazareti ndiye Masihi wa Ufalme. Tunajua kwamba Yesu ndiye kwa sababu ya yale aliyotenda kwa maskini na yale aliyowaambia maskini. Je, ni jinsi gani, basi, tunavyoweza kudhihirisha uhusiano wetu na Masihi? Kwa kuwapenda na kuwatendea wenye njaa, wenye kiu, walio uchi, wageni, wafungwa, na wagonjwa kana kwamba tunamtendea Yesu mwenyewe, maana kwa kweli, kile tunachowatendea (kwamba ni chema au kibaya) tunamtendea Yeye (Mt. 25:31 46). Enzi ya Masihi (na jamii ya Kimasihi) itajulikana kwa haki na uadilifu wake unaotendeka kwa niaba ya waliovunjika moyo na wahitaji. Hili ni muhimu kwetu leo. Masihi wa kweli alithibitisha sifa yake ya kiroho kwa upendo wake, ukarimu wake, utunzaji wake, na uponyaji kwa watu walio hatarini zaidi, wasiopendeza, na wenye uhitaji katika jamii ya Waisraeli, na kwa kuwahubiria maskini Habari Njema ya ujio wa Ufalme wa Mungu. Sasa wafuasi wake lazima wathibitishe uhalisia wao kwa kudhihirisha matendo yale yale kwa watu wa aina ile ile kama alivyofanya yeye. Hakika wale wanaodai kuwa wanakaa ndani yake imewapasa kuenenda kama yeye alivyoenenda (1 Yoh. 2:6). Hakika Yesu ndiye ambaye sisi sote tunamtazamia. Je, wewe ni sehemu ya jamii yake mpya ya Kimasihi ya milele? Kama vile wimbo fulani unaoimbwa wakati wa kuota moto kambini unavyosema, “Nao watajua sisi ni Wakristo kwa upendo wetu, kwa upendo wetu, ndiyo, watajua sisi ni Wakristo kwa upendo wetu.”
4
Made with FlippingBook Annual report maker