https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
/ 1 8 3
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
Baada ya kukiri na/au kuimba Kanuni ya Imani ya Nikea (iliyopo kwenye viambatisho), omba maombi yafuatayo: Ee Mungu, unawaalika maskini na wenye dhambi kuchukua nafasi zao katika kusanyiko la sherehe la agano jipya. Kanisa lako na liheshimu daima uwepo wa Bwana katika maisha ya wanyenyekevu na wanaoteseka, na tujifunze kutambuana kama kaka na dada, waliokusanyika pamoja kuzunguka meza yako. Tunaomba hayo kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo, anayeishi na kutawala pamoja nawe katika umoja wa Roho Mtakatifu, Mungu mmoja, milele na milele. Amina. ~ Presbyterian Church (U.S.A.) na Cumberland Presbyterian Church. Kitengo cha Huduma ya Theolojia na Ibada. Kitabu cha Ibada ya Pamoja . Louisville, KY: Westminister/John Knox Press, 1993. uk. 372.
Kanuni ya Imani ya Nikea na Maombi
Weka kando daftari lako na nyenzo za kujifunzia, kusanya pamoja mawazo yako, kisha ufanye Jaribio la Somo la 3, Utume wa Kikristo na Jiji.
Jaribio
Pitia pamoja na mwanafunzi mwenzako, andika na/au nukuu andiko la kukumbuka la kipindi kilichopita: Waebrania 11:13-16.
Mazoezi ya Kukariri Maandiko
4
Kusanya muhtasari wako wa kazi ya usomaji ya wiki iliyopita, yaani, jibu lako lenye maelezo machache kuhusu mambo muhimu uliyoyaona katika vitabu ulivyoelekezwa kusoma, kwa maneno mengine, zile hoja kuu ambazo waandishi walitaka kuziwasilisha (taz. Fomu ya Ripoti ya Usomaji).
Kazi za Kukusanya
MIFANO YA REJEA
Wanawezaje Kuishi Namna Ile?
Katika jamii ambayo inathamini bidii katika kazi, uzalishaji, na uwajibikaji binafsi, maskini «wenye uhitaji wa kweli» wana wakati mgumu kuonyesha kwamba wanastahili kusaidiwa na kuungwa mkono. Kwa ujumla, kuna mwelekeo wa kutowatazama maskini kwa misingi ya ukandamizaji wa kihistoria, mfumo wa sera za kijamii zinazofanya iwe vigumu kwao kushiriki katika shughuli za uzalishaji za jamii pana, au kutendewa vibaya na wale walio madarakani. Badala yake, katika utamaduni wa kawaida wa Marekani, mtu maskini anachukuliwa kwamba ni maskini kwa sababu ya kukosa uthubutu, kutokuwa na bidii ya kazi, kutojithamini, na utovu wa maadili. Ni kweli kwamba kuna watu wengi ambao ni maskini kwa sababu ya kushindwa kwao kimaadili, maamuzi mabaya ya kibinafsi, uraibu, au
1
Made with FlippingBook Annual report maker