https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

1 8 4 /

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

uvivu. Hata hivyo, inachukuliwa kwamba tabia hizi ndizo walizo nazo asilimia kubwa ya maskini walio wengi; na mara nyingi, sera na huduma kwa watu maskini hutegemea kile kinachoonekana kama ukosefu wa nidhamu wa watu maskini na kwamba hawana dhamira ya dhati ya kuboresha hali zao. Ni jambo la kawaida kabisa, hata katika mazingira ya Kikristo, kuwalaumu maskini kwa hali zao. Watu wenye mtazamo huu wanaamini kwamba kuna fursa nyingi zinazopatikana kwa mtu yeyote ambaye anataka kujiboresha na kuboresha hali yake ya maisha. Ikiwa mtu ni maskini kwa muda mrefu, ni kosa lake mwenyewe – hakuna sababu ya mtu yeyote kuendelea kuishi katika hali hiyo. Je, una mawazo gani kuhusu mtazamo huu ambao ni maarufu sana miongoni mwa tamaduni nyingi zisizo za Kikristo, za tabaka la kati, na hata miongoni mwa Wakristo pia? Katika kujadili suala la imani na wokovu, kumekuwa na swali kubwa ambalo limedumu katika historia ya Kikristo: «Imani inayookoa ni nini?» Tunajuaje kwamba mtu ametubu kihalali kutoka katika dhambi na ibada ya sanamu, na kumwamini Bwana Yesu Kristo? Katika historia ya mapokeo ya madhehebu ya Kiinjili, kwa kawaida tumekuwa tukitegemea viashiria vya nje wakati wa wokovu kutumika kama ushahidi wa imani ya kweli. Mtu kuinua mkono juu mwishoni mwa mahubiri, kusimama ili kuitikia mwaliko wa wokovu, akipita mbele na kuomba pamoja na mchungaji, na kuongozwa katika «Sala ya Toba,» yote hayo yametumika kama ushahidi thabiti wa imani iokoayo. Hata hivyo, ushahidi mwingi wa kibiblia hutokea muda mrefu baada ya ukiri wa kwanza wa imani. Mambo yanayotazamiwa ni je, mtu huyo anawapenda ndugu na dada zake katika Kristo (Yoh. 13:34-35)? Anaonyesha upendo halisi kwa wale ambao hawana chakula na nguo (Yak. 2:14-16)? Na je, amefungua moyo wake na kuwatendea mema wale wanaohitaji msaada (1 Yoh. 3:16-18)? Dini ya kweli, kwa mujibu wa Yakobo, ni kukidhi mahitaji ya wajane na yatima katika dhiki zao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa (Yak. 1:27). Je, unadhani ni kwa namna gani ushahidi wa kimapokeo wa madhehebu ya Kiinjilisti wa imani inayookoa unalingana na kile ambacho Biblia inasema hapa na mahali pengine kuhusu mwenendo na matendo yetu kwa maskini kama uthibitisho wa uhusiano wetu na Mungu? Dini ya Kweli

2

4

Mpe Ndoano!

Msemo wa zamani, «Mwenye njaa usimpe samaki, mpe ndoano» unachukuliwa karibu kote kuwa sera nzuri ya kijamii ya namna ya kuwatendea maskini. Wengi wanaamini kwamba mifumo ya ustawi wa jamii imeshindwa kwa sababu hii;

3

Made with FlippingBook Annual report maker