https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

/ 1 8 5

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

usaidizi endelevu wa kifedha ambao hauna masharti magumu ya jinsi fedha hizo zinavyopaswa kutumika huonekana kama njia ya kuendeleza hali ya utegemezi na kudhoofisha uwajibikaji wa watu binafsi. Kwa bahati mbaya, wengi ambao wamepokea misaada kwa kweli wamefikia kuiona serikali kama mfadhili wao, na hivyo kusababisha wengine kuacha kuajiriwa ili waendelee kupata msaada huo (hata kama ni kiasi kidogo sana). Sasa, mashirika mengi ya serikali na ya kijamii yameanza kuweka masharti magumu kuhusu urefu wa muda ambao mtu anaweza kupokea msaada wa serikali, na kufanya iwe jambo la lazima watu kupata mafunzo ya ujuzi wa kazi za mikono na kuingia katika ajira. Wanasema kwamba msaada ni suala la kuwezeshwa kwa muda si huduma ya kudumu. Wale wanaopinga aina hizi za mbinu wanadai kwamba ingawa mipango hii inaonekana kuwa ni mizuri, haishughulikii masuala ya msingi zaidi kama masuala ya kiwango cha mshahara kazini ambao unakidhi kuweza kusaidia familia inayokua. Manufaa ya muda mfupi ya kuweza kumwondoa mtu kwenye orodha ya misaada ya ustawi wa jamii huongeza tu tatizo kwenye swali la msingi zaidi la ikiwa tunaweza kurekebisha kwa haraka hali hii au tatizo hili la kijamii ambalo limejitengeneza kwa miaka mingi. Je, kwa maoni yako ni mtazamo upi unaopaswa kuwa mtazamo wa Kikristo unaoweza kutetewa na kusimamiwa na Wakristo kuhusu jukumu la serikali katika kusaidia maisha ya raia wake wenye uhitaji zaidi?

4

Utume wa Kikristo na Maskini Sehemu ya 1: Shalom katika Jamii ya agano

YALIYOMO

Mchungaji Dkt. Don L. Davis

Dhana ya maskini imejengwa juu ya maono ya kibiblia ya shalom, au ukamilifu: shalom ni neno la Kiebrania linalomaanisha «ukamilifu wa jamii ya wanadamu katika ushirika na Mungu na baina yao mmoja kwa mwingine.» Vipengele vya kibiblia vya shalom ni pamoja na uzima na afya njema, usalama na ulinzi, maelewano kati ya majirani, ustawi na utoshelevu wa mali, na kukosekana kwa uovu na migogoro – Amani ya kweli na kamilifu. Hili pia linajumuisha wazo la shalom kama utoaji wa Mungu kwa msingi wa neema yake, unaohusishwa na ujio wa Masihi ambaye ni Mfalme wa shalom, pamoja na shalom kama kiwango cha maisha kwa watu wa Mungu. Umaskini ni kunyimwa shalom ya Mungu; baraka na upaji wake vilitolewa ili kuzuia kutokea kwa umaskini, na amri na maagizo ya Mungu kwa jamii ya agano zilikusudiwa kuhakikisha haki na uadilifu kati ya watu wa Yehova. Tukio la “Kutoka” lilijumuisha utambulisho wa Mungu pamoja na maskini na walioonewa, likifunua moyo wake wa haki na kuunda jamii yake ya agano ambayo iliitwa kuwa kielelezo cha utakatifu wake, taswira ya haki na rehema zake, na nuru kwa mataifa.

Muhtasari wa Sehemu ya 1

Made with FlippingBook Annual report maker