https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

/ 1 8 7

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

tukio muhimu ambalo linajumuisha utambulisho wa Mungu na maskini na walioonewa, akifunua moyo wake wa haki na kuunda jamii yake ya agano ambayo iliitwa ili iweze kuwa ni kielelezo cha utakatifu wake, taswira ya haki na rehema zake, na nuru kwa mataifa. • Maandiko yamefafanua sababu kadhaa za umaskini, kutia ndani majanga ya asili na misiba (k.m., njaa, ukame, vimbunga, n.k.), uvivu na uzembe wa watu binafsi (k.m., maamuzi mabaya, tabia mbaya, uvivu, mioyo migumu, n.k.), na uonevu na matendo ya ukosefu wa haki yanayotendwa na watu wenye nguvu (k.m., unyanyasaji, unyonyaji, nk). Neno “maskini” katika Maandiko linahusianishwa na dhana mbalimbali zinazotumika kama visawe, kutia ndani “mjane,” “yatima,” na “mgeni.” • Viwango vya agano la Mungu vya namna ya kuwatendea maskini kwa ukarimu na haki vinatumika kama kielelezo cha moyo wake mwenyewe kwa ajili yao. Aliweka sheria maalum kwa ajili ya kuwatunza maskini ambazo ziliwekwa katika maagizo ya Sheria (Torati) kuhusu masharti ya mavuno na masazo yake, na haki katika mahakama ambapo mambo yote, hatua zote, na shughuli zote zilipaswa kufanyika kwa uaminifu na haki. Rasilimali za Watu wa Mungu zilipaswa kugawanywa katika mwaka wa Sabato, na maskini wakipewa sehemu ya mazao ya mashamba na mizabibu. • Watu wa Mungu walikatazwa kutoza riba kwa maskini, na kuagizwa kulipa malipo ya haki na kwa wakati kwa ajili ya kazi ya siku moja (yaani, mshahara au posho kulipwa siku hiyo hiyo bila ukandamizaji au ulaghai wowote). Waliagizwa kuwatendea maskini kwa ukarimu wa kiwango cha juu (“sera ya mkono wazi”), na kutenga rasilimali kwa ajili yao (sehemu ya zaka na fadhila kutolewa kwa wahitaji na watu walio hatarini zaidi katikati ya jamii). Maskini walipaswa kujumuishwa katika sherehe na siku kuu zote, na katika mwaka wa Yubile, maskini walipaswa kurejesha (kukomboa) mashamba yao na mali zao, pamoja na wale ambao hawakuwa na fedha za kutosha kukomboa mali zao. • Maana ya viwango hivi kwa jamii ya agano la Mungu iko wazi: katika shughuli zao zote, Watu wa Mungu walipaswa kuakisi moyo wa Mungu kwa maskini, kwa msingi wa ukombozi wa Mungu kwao katika “Kutoka”, na walipaswa kuonyesha shalom ya Bwana katika mahusiano yao yote na kushughulika kwao na watu wengine.

4

Made with FlippingBook Annual report maker