https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
1 8 8 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
I. Dhana ya maskini katika Agano la Kale
Muhtasari wa Sehemu ya Kwanza ya Video
A. Jamii ya ufalme wa Mungu na ukamilifu ( shalom ).
1. Shalom (ukamilifu) ni neno la Kiebrania linalomaanisha «ukamilifu wa jamii ya wanadamu katika ushirika na Mungu na baina yao mmoja kwa mwingine.»
Umaskini Haujawahi Kuwa Mapenzi ya Mungu
Umaskini kama hali halisi ya kijamii kamwe hauchukuliwi kama hali inayofaa katika Agano la Kale. Umaskini ni uhitaji, dhiki na mateso, na ni kinyume na mapenzi ya Mungu. «Lakini (kwa kuwa Bwana atakubarikia kweli katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako, uimiliki, iwe urithi wako)» (Kum. 15:4). Umaskini ni laana; ustawi na mafanikio ni baraka kutoka kwa Mungu. Lakini baraka za Mungu zinapaswa kusababisha ukarimu na utunzaji hawatakuwako maskini kwenu; wa watu maskini (Kum. 15:7-11). ~ Hans Kvalbein. “Poverty.” The New Dictionary of Biblical Theology. T. D. Alexander, mh. (toleo la kielektroniki). Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 2001 .
2. Ukamilifu au shalom ni dhana yenye kina cha utajiri mkubwa wa maana, inayojumuisha ukamilifu uliojaa uhalisia na baraka.
a. Inajumuisha afya na uzima, Mwa. 43:28.
b. Inahusisha usalama (ulinzi dhidi ya maumivu na madhara), Zab. 4:8.
4
c. Inahusisha maelewano na kukubaliana kati ya majirani, 1 Sam. 16:4.
d. Inahusisha ustawi na utoshelevu wa mali, Zab. 73:3.
e. Inahusisha kutokuwepo kwa uovu na migogoro, bali amani ya kweli, Zab. 120:7.
3. Shalom inahusishwa moja kwa moja na maisha ya jamii ya agano katika uhusiano sahihi na Mungu. Ni matokeo ya riziki yake ya neema.
4. Masihi alitabiriwa kwamba atakuwa Mfalme wa shalom akileta shalom ya milele katika Ufalme wa Mungu chini ya utawala wake wa haki, Isa. 9:6-7.
Made with FlippingBook Annual report maker