https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

/ 1 8 9

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

5. Kwa hiyo, kiwango cha Mungu kwa watu wake ni kusimama kinyume na kuzuia chochote ambacho kingeingilia nia yake ya amani miongoni mwa watu wake.

B. Umaskini kama kukosekana kwa shalom ya Mungu.

1. Baraka za Bwana zilikusudiwa kuzuia kutokea kwa umaskini miongoni mwa watu wake, Kum. 15:4-5.

2. Utii kwa amri na viwango vya Mungu ungehakikisha haki na uadilifu katika jamii ya agano.

a. Isa. 58:10-11

b. Mit. 28:27

4

C. Uaminifu kwa agano: wajibu wa watu wa Mungu kwa ajili ya kuendeleza shalom .

1. Shalom ya Bwana ilikuwa zawadi, lakini jitihada za kutafuta ustawi wa wengine zilitegemea utii wao wa kuwajibika kwa mapenzi ya Mungu, Kum. 28:1-8.

2. Kutii sauti ya Mungu na kushika agano lilikuwa sharti la kupata baraka na utunzaji wa Mungu, Kut. 19:5-6.

3. Kutengwa huku kwa ajili ya kufanya mapenzi na maagizo ya Bwana kulihusiana moja kwa moja na uhusiano wa jamii ya agano na Mungu, Law. 11:44-45.

Made with FlippingBook Annual report maker