https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
1 9 0 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
II. Utambulisho wa Mungu na maskini
Mungu Hujitambulisha na Watu Maskini Vitabu vya unabii mara nyingi vinawashutumu matajiri kwa kuwadhulumu maskini (Amosi 8:4-6; Isa. 10:1-4; 32:6 7; Mika 3:1-4; Yer. 5:26-29; Eze. 18:12 13 ). Uchamungu wa kweli unajumuisha kuwajali maskini, na kufunga kwa kweli ni pamoja na kugawana mkate na wenye njaa (Isa. 58:5-10). Fasihi ya hekima ina matangazo yote mawili ya baraka za Mungu kwa wale wanaowajali wasio na msaada (Mit. 14:21, 31; 19:17; 22:9; 28:8; 31:20; Mhu. 11:1) na maonyo dhidi ya kufunga sikio na kukunja mkono mbele ya uhitaji wa maskini (Mit. 21:13; 28:27). Mungu ndiye mlinzi wao, na wale wanaowadhihaki au kuwaonea maskini wanamtukana muumba wao (Mit. 14:31; 17:5). ~ Hans Kvalbein. “Poverty.” The New Dictionary of Biblical Theology. T. D. Alexander,
A. Maandiko kuhusu utambulisho wa Mungu na maskini.
1. Mungu Mkuu wa historia anafanya kazi ya kuwainua na kuwabariki maskini na waliokandamizwa, Kut. 3:7-8; 6:5-7; Kumb. 6:6-8.
2. Mungu atasimama dhidi ya mtu mdhalimu kuwakomboa na kuwabariki wale wanaokandamizwa na kuangamizwa kwa sababu ya shida zao.
a. Zab. 12:5
b. Zab. 10:12
4
c. Rej. Yer. 5:26-29; Zab. 10; Isa. 3:14-25; Yer. 22:13-19; Amosi 5:11; 6:4; 7:11, nk.
3. Utambulisho wa Mungu na maskini una nguvu sana, Mit. 14:31; 19:17.
4. Mungu anadai kwamba jamii ya agano ionyeshe kuwajali waliovunjika moyo, maskini, na waliokandamizwa, kama ambavyo Yeye Mungu anafanya, Kut. 22:21-24, taz., Kum. 15:13-15.
mh. (toleo la kielektroniki). Downers Grove, IL: IVP, 2001 .
Made with FlippingBook Annual report maker