https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
/ 1 9 7
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
I. Kupewa haki ya kumiliki rasilimali za uzalishaji : katika mwaka wa Yubile, maskini walipaswa kurejeshewa (kukomboa) mali zao.
1. Urejesho wa mali ulipaswa kufanyika kwa haki na uadilifu, Law. 25:13-17.
2. Sheria iliwekwa kwa ajili ya wale ambao fedha na rasilimali zao hazikutosha kukomboa mali zao na kuzirejesha, Law. 25:25-28.
V. Dondoo za mwisho za kiwango cha Mungu katika jamii ya agano: Ishi kwa kudhihirisha Shalom ya Mungu katikati ya Jamii ya agano.
Kumb. 15:4-5 Lakini hawatakuwako maskini kwenu; (kwa kuwa Bwana atakubarikia kweli katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako, uimiliki, iwe urithi wako;) 5 kwamba utaisikiza tu kwa bidii sauti ya Bwana, Mungu wako, uyatunze maagizo haya yote nikuagizayo leo, kuyafanya..
Maskini katika Agano la Kale: Muhtasari
Kwa nama fulani imeonekana kwamba Mungu aliwafanikisha wenye haki kwa mali (Zab. 112:1-3). Ingawa ni kweli kwamba faida za kufanya kazi kwa bidii na kuwa na nidhamu ya matumizi zinaonekana wazi wazi kwa watu binafsi na kwa taifa, na kwamba Mungu ameahidi kuwabariki wale wanaoshika amri zake (Kum. 28:1-14), kulikuwa na idadi ya watu maskini katika Israeli katika kila kipindi cha historia ya taifa hilo. Umaskini wao unaweza kuwa ulisababishwa na majanga ya asili ambayo yalisababisha kukosekana kwa mavuno, inawezekana waliingia katika umaskini kwa sababu ya uvamizi wa adui, ukandamizaji wa majirani wenye nguvu au kupitia riba za kinyonyaji. Kulikuwa na wajibu kwa wanajamii wenye mali kuwategemeza ndugu zao maskini zaidi (Kum. 15:1-11). Waliokuwa katika hatari kubwa ya kuingia katika hali ya umaskini walikuwa ni yatima na wajane na wageni wasio na ardhi (walioitwa kwa Kiebrania gerim). Watu wa makundi hayo mara nyingi walikuwa wahasiriwa wa ukandamizaji (Yer. 7:6; Amosi 2:6-7a), lakini Yehova alikuwa mtetezi wao (Kum. 10:17-19; Zab. 68:5-6). Sheria iliamuru kwamba mpango ufanyike kwa ajili yao (Kum. 24:19-22), na pamoja nao walihesabiwa Walawi (Kum. 14:28-29) kwa sababu hawakuwa na ardhi. Mtu angeweza kujiuza utumwani, lakini ikiwa alikuwa Mwebrania ilimbidi atendewe tofauti na mgeni (Law. 25:39-46). ~R. E. Nixon. “Poverty.” The New Bible Dictionary . D. R. W. Wood, mh. Toleo la 3. (toleo la kielektroniki). Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 1996. uk. 945. .
4
Made with FlippingBook Annual report maker