https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
1 9 6 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
2. Hakuna ruhusa wala mwanya wa uonevu au wizi, Law. 19:13.
F. Fungua mikono, fungua moyo daima kwa maskini : ukarimu mkubwa ulipaswa kutendeka kwa yeyote aliyepatikana kuwa maskini au mhitaji, Kum. 15:7-11.
1. Pasiwe na ugumu wa moyo au chuki juu ya maskini katika nchi.
2. Kinachoshughulikiwa hapa ni msukumo wa ndani: Mfumbulie kwa kweli mkono wako nduguyo, mhitaji wako, maskini wako, katika nchi yako, Kum. 15:11.
G. Rasilimali zilizotengwa kwa ajili ya maskini : sehemu fulani za zaka zilipaswa kutolewa kwa maskini, ambazo zilifungamanishwa moja kwa moja na baraka za Mungu juu ya maisha na mazao yao.
4
1. Zaka na mahitaji yatolewe ili kukidhi mahitaji ya makuhani, pamoja na “mgeni, yatima, na mjane” (yaani, watu walio hatarini zaidi katika jamii ya agano), Kum. 14:28-29.
2. Kuweka kando fadhila kwa ajili ya kuwagawia walio hatarini kulihusishwa moja kwa moja na uhusiano wa mtu na Mungu na jamii yenyewe ya agano, Kum. 26:12-15.
H. Sikukuu na Sherehe, pia : maskini walipaswa kujumuishwa katika karamu na sherehe pamoja na watu wa Mungu.
1. Sikukuu ya Majuma, Kumb. 16:10-12.
2. Sikukuu ya Vibanda, Kumb. 16:13-14.
Made with FlippingBook Annual report maker