https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

/ 1 9 5

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

1. Utendaji wa mahakama uwe wa haki, uaminifu, na unaofuata ukweli wa jambo, bila kujali hadhi, heshima au nafasi ya mtu katika jamii, Kut. 23:2-3, Law. 19:15; Kumb. 10:17-18.

2. Vipimo viwe vya uaminifu katika shughuli zote za kibiashara, Law. 19:35-36, Mit. 11:1, Amosi 8:5.

C. Rasilimali za pamoja : katika mwaka wa Sabato, maskini walipewa sehemu ya mazao ya mashamba na mizabibu.

1. Hakuna mgeni ambaye angedhulumiwa au kuumizwa kwa namna yoyote katika jamii ya agano, Kut. 23:9-11.

2. Kwa mwaka wa Sabato, maandalizi yalipaswa kufanywa kwa ajili ya watumwa na wageni kustarehe pamoja na familia, Law. 25:3-6.

4

D. Kukatazwa kwa riba : watu wa Mungu walikatazwa kutoza riba, na nguo zilizowekwa rehani zilipaswa kurudishwa kabla ya jua kuzama.

1. Hakuna kudai au kuchukua riba kutoka kwa watu maskini, Kut. 22:25-27.

2. Mavazi yaliyowekwa rehani (kama dhamana ya mkopo) yalipaswa kurudishwa siku ile ile “jua lituapo,” Kum. 24:10-13.

E. Malipo ya haki, ndani ya muda mwafaka kwa kazi ya siku : posho au mshahara ulipaswa kulipwa kwa mfanyakazi wa siku (kibarua wa kutwa) kabla ya jua kutua.

1. Mshahara kulipwa siku hiyo hiyo, kabla ya jua kutua, Kum. 24:14-15.

Made with FlippingBook Annual report maker