https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

1 9 4 /

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

D. Muhtasari

Amri za A.K. Zilizoundwa ili Kupambana na Umaskini

“Katika Agano la Kale, neno ‘maskini’ linaweza kutafsiriwa kwa istilahi kuu sita na nyingine tatu – jumla ya marejeo 300, na kufunua uelewa mpana wa sababu, ukweli, na matokeo ya umaskini. Mtu maskini ni aliyekandamizwa, anayefedheheshwa, anayeonewa; mtu anayeomba na kulia kwa ajili ya haki; mnyonge au asiyejiweza; fukara; mhitaji, mtu tegemezi; na yule anayetawaliwa kwa nguvu chini ya mamlaka ya mtesi. Upeo mpana wa maneno (istilahi) unaonyesha kwamba ‘maskini’ anatazamwa katika mitazamo mingi tofauti. Maneno mengine yanayohusishwa kwa karibu sana na neno ‘maskini’ ni kama ‘mjane,’ ‘yatima’ na ‘mgeni.’” ~“Christian Witness to the Urban Poor.”

Ni dhahiri kwamba amri nyingi katika torati zilikusudiwa kuwasaidia maskini. Katika Kumbukumbu la Torati amri ya Sabato ina mwelekeo wa kijamii: haki ya kupumzika siku ya Sabato pia ni kwa ajili ya watumishi [yaani watumwa na wajakazi] kadhalika na wageni (Kum. 5:12-15). Wakati wa mavuno, waliagizwa wasivune kabisa mazao yaliyopo kwenye pembe za shamba, bali wayaache kwa ajili ya watu wahitaji. Vivyo hivyo, masazo ya mavuno yote yalipaswa kuachwa kwa ajili ya maskini (Law. 19:9-10; Kum. 24:17-22). Sheria inakataza mkopeshaji kuchukua riba au vazi kutoka kwa maskini anaowadai (Kut. 22:25-27; Kumb. 24:12-13). Katika Kumbukumbu la Torati 14:28-29 na 26:12 kuna maagizo ya zaka maalum kwa ajili ya maskini, kwa faida ya Mlawi, mgeni, yatima na wajane. Katika mwaka wa sabato nchi iliachwa bila kulimwa ili maskini wapate kuvuna na kula mazao ambayo yaliota yenyewe humo (Law. 25:1-7; Kum. 15:1-11). ~ Hans Kvalbein. “Poverty.” The New Dictionary of Biblical Theology. T. D. Alexander, mh. (toleo la kielektroniki). Downers Grove, IL: IVP, 2001.

Report of the Consultation of World Evangelization Mini-Consultation on Reaching the Urban Poor. Kamati ya Lausanne ya Uinjilishaji Ulimwenguni, 1980.

IV. Viwango vya jamii ya agano la Mungu: Kuwa kielelezo kama watu wa Mungu Kama jamii ya agano la Mungu mwenyewe, watu wa Israeli walikuwa chini ya wajibu wa kuonyesha uhuru, ukamilifu, na haki ya Bwana Mungu, ambaye sheria zake za haki zilikuwa kwa ajili ya ulinzi, ustawi, na baraka (shalom) kwa watu wa Mungu.

4

A. Sheria zilizowekwa kwa ajili ya kuwasaidia maskini : mazao ya mashamba hayakupaswa kuvunwa yote ili kuwaruhusu maskini kuokota masazo ya mavuno.

1. Msivune mpaka ukingo wa mashamba yenu kwa ajili ya maskini, Law. 19:9-10.

2. Msirudie (kuvuna tena) mashamba yenu, Kum. 24:19-22.

B. Haki katika mahakama : Jamii ya agano ya Mungu ilipaswa kusisitiza haki katika shughuli zote za kibiashara na za kisheria.

Made with FlippingBook Annual report maker