https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

2 6 8 /

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

KIAMBATISHO CHA 21 Nafasi ya Wanawake katika Huduma Dkt. Don L. Davis

Ingawa ni wazi kwamba Mungu ameweka utaratibu uliopangwa wazi wa wajibu ndani ya nyumba, ni wazi vile vile kwamba wanawake wameitwa na kupewa karama na Mungu, wakiongozwa na Roho wake mwenyewe kuzaa matunda yanayopasa wito wao katika Kristo. Katika Agano Jipya, amri zinaelekezwa haswa kwa wanawake kutii, na kitenzi mahususi cha Kiyunani hupotasso , kikitokea mara kwa mara ambacho kinamaanisha “kuweka chini ya” au “kunyenyekea” (taz. 1 Tim. 2:11). Neno pia lililotafsiriwa katika neno la Kiingereza “ subjection ” (kutawaliwa) linatokana na mzizi huo huo mmoja. Katika mazingira kama haya tafsiri hizi za Kiyunani hazifai kueleweka kwa njia nyingine yoyote isipokuwa kama maonyo chanya kuhusiana na mfumo wa kimungu uliowekwa kwa ajili ya nyumba, ambapo wanawake wameagizwa kujifunza kwa utulivu na utii, kuamini na kufanya kazi ndani ya mpango wa Bwana mwenyewe. Utaratibu huu wa utii wa mwanamke nyumbani, hata hivyo, haupaswi kutafsiriwa vibaya kumaanisha kwamba wanawake wamekataliwa kuhudumu katika karama zao chini ya uongozi wa Roho. Hakika, ni Roho Mtakatifu kwa njia ya upaji wa neema ya Kristo ambaye hugawa karama kama apendavyo, kwa ajili ya kulijenga Kanisa (1 Kor. 12:1-27; Efe. 4:1-16). Vipawa havitolewi kwa waamini kwa vigezo vya jinsia; kwa maneno mengine, hakuna dokezo katika Maandiko kwamba baadhi ya vipawa ni kwa ajili ya wanaume tu, na vingine ni kwa ajili ya wanawake tu. Kinyume chake, Paulo anathibitisha kwamba Kristo alitoa karama kama matokeo ya moja kwa moja ya ushindi wake dhidi ya shetani na wafuasi wake (rej. Efe. 4:6-). Hili lilikuwa ni chaguo lake binafsi, lililotolewa na Roho wake kwa yeyote kama atakavyo (rej. 1Kor. 12:1-11). Katika kuthibitisha huduma ya wanawake tunathibitisha haki ya Roho ya kuwa mbunifu kwa watakatifu wote kwa ajili ya ustawi wa watu wake wote na upanuzi wa Ufalme wake, kama yeye aonavyo inafaa, na si lazima iwe kama sisi tuamuavyo (Rum. 12:4-8 ; 1 Pet. 4:10-11). Zaidi ya hayo, uchunguzi wa kina wa Maandiko kwa ujumla unaonyesha kwamba kitendo cha Mungu kuweka mpangilio au utaratibu katika nyumba hakiathiri kwa namna yoyote kusudi lake kwa wanaume na wanawake kumtumikia Kristo wakiwa wanafunzi na watenda kazi pamoja, chini ya uongozi wa Kristo. Fundisho la wazi katika Agano Jipya la Kristo kama kichwa cha mwanamume, na mwanamume kama kichwa cha mwanamke ( ona 1 Kor. 11:4) linaonyesha heshima ya Mungu kwa uwakilishi wa kiroho ndani ya nyumba. Kukatazwa kwa wanawake kushika nyadhifa za kufundisha/kutawala kunaonekana kuwa ni onyo la kulinda mfumo

Made with FlippingBook Annual report maker