https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

/ 2 6 9

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

Nafasi ya Wanawake katika Huduma (muendelezo)

wa mamlaka na wajibu ambao Mungu aliuweka ndani ya nyumba. Kwa mfano, neno mahususi la Kiyunani katika kifungu kinachojadiliwa sana cha 1 Timotheo 2:12, andros , ambalo mara nyingi limetafsiriwa “mwanamume,” linaweza pia kutafsiriwa “mume.” Basi, kwa tafsiri hiyo, fundisho lingekuwa kwamba mke hapaswi kumtawala mume wake. Fundisho hili la mwanamke ambaye, kwa kuchagua kuolewa, anakubali kuwa mtii kwa hiari “kupanga mstari chini ya” mume wake, linakubaliana kabisa na kiini cha mafundisho ya Agano Jipya juu ya jukumu la mamlaka katika nyumba ya Kikristo. Neno la Kiyunani hupotasso , linalomaanisha pia “kupanga mstari chini ya” hurejelea utii wa hiari wa mke kwa mume wake mwenyewe (rej. Efe. 5:22, 23; Kol. 3:18; Tito 2:5; 1 Pet. 3:1). Hili halihusiani na hadhi yoyote ya juu au uwezo wa mume; badala yake, hili linarejelea mpango wa Mungu wa ukichwa wa kimungu, mamlaka ambayo hutolewa kwa ajili ya faraja, ulinzi, na huduma, si kwa ajili ya uharibifu au utawala (rej. Mwa. 2:15-17; 3:16; 1 Kor. 11:3). Kwa hakika, kitendo cha ukichwa huu kufasiriwa katika mwanga wa ukichwa wa Kristo juu ya Kanisa kinaashiria aina ya ukichwa wa kimungu ambao unapaswa kuwepo, yaani ile hali ya utunzaji, utumishi, na ulinzi usiochoka ambao ni jukumu la uongozi wa kimungu. Bila shaka, kuaswa kama huko kwa mke kujitiisha kwa mume hakungekataza kwa njia yoyote kwamba wanawake wasishirikishwe katika huduma ya kufundisha (k.m., Tito 2:4), bali, badala yake, kwamba katika suala mahususi la wanawake walioolewa, kwamba huduma zao zinapaswa kuwa chini ya ulinzi na mwongozo wa waume zao (Mdo. 18:26). Hili lingedai kwamba huduma ya mwanamke aliyeolewa kanisani ipewe uangalizi na mume wake kwa ajili ya ulinzi na usaidizi pale inapohitajika, si kwa sababu ya dhana yoyote ya uwezo duni au kasoro katika maisha ya kiroho, bali, kama mfafanuzi mmoja alivyoliweka, kwa ajili ya “kuepuka utata na kudumisha utaratibu” (rej. 1Kor. 14:40). Katika miji ya Korintho na Efeso (ambayo ililengwa moja kwa moja na maelekezo ya waraka kwa Wakorintho na kwa Timotheo), inaonekana kwamba kizuizi cha Paulo juu ya ushiriki wa wanawake kilichochewa na matukio ya hapa na pale, masuala ambayo yalijitokeza hasa kutokana na mazingira ya miji hiyo, na kwa hiyo kinakusudiwa kueleweka katika miktadha hiyo. Kwa mfano, mtihani wenye utata mkubwa wa wanawake kukaa “kimya” katika kanisa (ona 1 Kor. 14 na 1 Tim. 2) hauonekani kwa njia yoyote ile kudhoofisha jukumu kuu ambalo wanawake walikuwa nalo katika upanuzi wa Ufalme na maendeleo ya Kanisa katika karne ya kwanza. Wanawake walihusika katika huduma za unabii na maombi (1Kor.

Made with FlippingBook Annual report maker