https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

2 7 0 /

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

Nafasi ya Wanawake katika Huduma (muendelezo)

11:5), kuelekeza na kulea watu binafsi (Mdo. 18:26), mafundisho (Tito 2:4, 5), kushuhudia (Yoh. 4:28, 29), kukirimu (Mdo. 12:12) kama watenda kazi pamoja na mitume katika kazi ya Injili (Flp. 4:2-3). Paulo hakuwaweka wanawake katika nafasi ya chini au hadhi iliyofichwa bali alitumika bega kwa bega na wanawake kwa ajili ya Kristo: “Namsihi Euodia, namsihi na Sintike, wawe na nia moja katika Bwana. Naam, nataka na wewe pia, mjoli wa kweli, uwasaidie wanawake hao; kwa maana waliishindania Injili pamoja nami , na Klementi naye, na wale wengine waliotenda kazi pamoja nami, ambao majina yao yamo katika kitabu cha uzima” (Flp. 4:2-3). Zaidi ya hayo, ni lazima tuwe waangalifu kutofautisha kutweza utu wa wanawake (yaani, asili yao kama wanawake) na nafasi yao ya usaidizi katika uhusiano wa ndoa. Licha ya maelezo ya wazi ya jukumu la wanawake kama warithi wenye hadhi sawa wa neema ya uzima katika uhusiano wa ndoa (1 Pet. 3:7), ni wazi vile vile kwamba Ufalme wa Mungu umeleta badiliko kubwa kuhusiana na namna wanawake wanavyopaswa kutazamwa, kueleweka, na kukumbatiwa katika jamii ya Ufalme. Ni wazi kwamba katika Kristo sasa hakuna tofauti kati ya tajiri na maskini, Myahudi na Myunani, mgeni na mshenzi, mtumwa na mtu huru, na vilevile mwanamume na mwanamke (taz. Gal. 3:28; Kol. 3:11). Wanawake waliruhusiwa kuwa wanafunzi wa Rabi (ambalo lilikuwa jambo geni na lisilokubalika wakati wa Yesu), na walitekeleza majukumu muhimu katika kanisa la Agano Jipya, ikijumuisha kuwa watenda kazi bega kwa bega na mitume katika huduma (k.m., ona Euodia na Sintike katika Flp. 4:1-), pamoja na kukaribisha kanisa kukusanyika katika nyumba zao (rej. Fibi katika Rum. 16:1-2, na Afia katika Flm. 1). Kuhusiana na suala la mamlaka ya kichungaji, ninaamini kwamba kwa uelewa wa Paulo, jukumu la kuwakamilisha watakatifu (ambapo mchungaji-mwalimu ni jukumu mojawapo, rej. Efe. 4:9-15) si mahususi kwa jinsia fulani. Kwa maneno mengine, maandiko yanayotoa maelekezo na yenye kauli ya mwisho, kwa mtazamo wangu, kuhusiana na utendaji wa karama na nyadhifa na kazi za ofisi za kihuduma ni maandiko ya Agano Jipya ambayo yanahusu karama (1Kor. 12:1-27; Rum. 12:4-8; 1 Pet. 4:10-11, na Efe 4:9-15). Hakuna dalili katika andiko lolote kati ya hayo inayodokeza kwamba karama fulani ni mahususi kwa jinsia fulani. Kwa maneno mengine, ili kujenga hoja yenye mashiko thabiti kwamba wanawake hawakuruhusiwa kamwe kuwa katika majukumu ambayo kwa asili yalihusiana na uchungaji au kuwakamilisha watakatifu, hoja rahisi na yenye ufanisi zaidi itakuwa kuonyesha kwamba Roho Mtakatifu hangeweza kamwe kufikiria kumpa mwanamke karama isipokuwa tu zile zinazofaa kwa aina za wito ambazo alihisi

Made with FlippingBook Annual report maker