https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

/ 2 7

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

I. Prolegomena juu ya utume: Picha kubwa

Muhtasari wa Sehemu ya Kwanza ya Video

Utume wa Mungu unahusu Mwili wa Kristo, Mwili wa ulimwengu mzima.

Hivyo basi, mwili wa Yesu uliosulubishwa na mwili wa kikanisa, kanisa, haiwezi kutenganishwa. Kuna matokeo kadhaa yanayotiririka kutokana na maana ya picha hii. Kwanza, ingawa, ni lazima tutambue kwamba katika nyaraka za awali, hasa Wakorintho na Warumi, msisitizo ni kuhusu kanisa la mahali pamoja, namna ambavyo katika umoja wake linamdhihirisha Kristo aliyesulubiwa na aliye hai. Lakini katika nyaraka za baadaye, Wakolosai na Waefeso, picha hiyo imepanuliwa wigo wake ili kulijumuisha kanisa la ulimwengu wote (Kol. 1:18; 2:19; Efe. 1:22-23; 4:16). Kristo ndiye “Kichwa” cha mwili ambao ni zaidi ya jumuiya ya imani ya mahali pamoja, na mabadiliko haya ya taswira yana umuhimu mkubwa, kwa sababu yanatoa maono au picha ya kanisa ambalo Injili yake “inazidi kuzaa matunda na kuenea ulimwenguni kote” (Kol. 1:6), wito wa utume ambao angalau ni wa lazima kama wito wa kujenga maisha ya jumuiya ya imani ya mahali pamoja. ~ Leland Ryken. Dictionary of Biblical Imagery . (toleo la kielektroniki) Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 2000, uk. 109.

1

A. Ufafanuzi: Utume ni tangazo la fursa ya wokovu na ukombozi wa Mungu kwa njia ya Yesu Kristo na kazi yake katika uwezo wa Roho Mtakatifu kwa makundi yote ya watu.

1. Tangazo la fursa ya wokovu na ukombozi wa Mungu: utume unahusu makusudi ya Mungu na fursa yake aliyoitoa ya neema na msamaha.

a. 2 Timotheo 1:8-10

b. Warumi 5:8

c. Waefeso 1:6-8

Made with FlippingBook Annual report maker