https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
/ 3 0 7
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
Ili Tuwe Umoja (muendelezo)
sababu ya ushirika wenu katika kuieneza Injili, tangu siku ile ya kwanza hata leo hivi. 2. Epafrodito alikuwa mjumbe wao aliyepeleka misaada yao kwa Paulo , Flp. 2:25 – Lakini naliona imenilazimu kumtuma kwenu Epafrodito, ndugu yangu, mtenda kazi pamoja nami, askari pamoja nami; tena ni mtume wenu na mhudumu wa mahitaji yangu. 3. Wafilipi walishiriki kikamilifu katika kusaidia huduma ya Paulo tangu mwanzo , Flp. 4:15-18 – Nanyi pia, ninyi wenyewe mnajua, enyi Wafilipi, ya kuwa katika mwanzo wa Injili, nilipotoka Makedonia, hakuna kanisa lingine lililoshirikiana nami katika habari hii ya kutoa na kupokea, ila ninyi peke yenu. 16 Kwa kuwa hata huko Thesalonike mliniletea msaada kwa mahitaji yangu, wala si mara moja. 17 Si kwamba nakitamani kile kipawa, bali nayatamani mazao yanayozidi kuwa mengi, katika hesabu yenu. 18 Lakini ninavyo vitu vyote na kuzidi, tena nimejaa tele; nimepokea kwa mkono wa Epafrodito vitu vile vilivyotoka kwenu, harufu ya manukato, sadaka yenye kibali, impendezayo Mungu. III. Ushirikiano 3 Unahusisha Kushirikiana Pamoja kama Watenda Kazi Wenza na Washirika Wenza Katika Kazi ya Kuendeleza Ufalme: Tunalo Kusudi Moja na Kazi Moja. A. Ushirikiano unahusisha kila mtu na kila kusanyiko kuleta mezani uzoefu wao wa kipekee, mtazamo, na karama kwa ajili ya matumizi ya wote , Gal. 2:6-8 – Lakini wale wenye sifa ya kuwa wana cheo; (walivyokuwa vyo vyote ni mamoja kwangu; Mungu hapokei uso wa mwanadamu); nasema, hao wenye sifa hawakuniongezea kitu; 7 bali, kinyume cha hayo, walipoona ya kuwa nimekabidhiwa injili ya wasiotahiriwa, kama vile Petro ya waliotahiriwa; 8 (maana yeye aliyemwezesha Petro kuwa mtume wa waliotahiriwa ndiye aliyeniwezesha mimi kwenda kwa Mataifa). B. Ushirikiano wa kweli unahusisha kutambua uongozi wa Bwana, fursa, na baraka anazotoa kwa wale walioitwa kuwakilisha maslahi yake katika maeneo ambayo amewaongoza , Gal. 2:9-10 – tena walipokwisha kuijua ile neema niliyopewa; Yakobo, na Kefa, na Yohana, wenye sifa kuwa ni nguzo, walinipa mimi na Barnaba mkono wa kuume wa shirika; ili sisi tuende kwa Mataifa, na wao
Made with FlippingBook Annual report maker