https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

3 0 8 /

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

Ili Tuwe Umoja (muendelezo)

waende kwa watu wa tohara; 10 ila neno moja tu walitutakia, tuwakumbuke maskini; nami neno lilo hilo nalikuwa na bidii kulifanya. C. Ushirikiano katika suala la kufanya kazi pamoja na kushirikiana pamoja unahusisha maono ya pamoja na kujitolea kwa jambo moja , kwa mfano, Timotheo, Flp. 2:19-24 – Walakini natumaini katika Bwana Yesu kumtuma Timotheo afike kwenu karibu, nifarijiwe na mimi, nikiijua hali yenu. 20 Maana sina mtu mwingine mwenye nia moja nami, atakayeiangalia hali yenu kweli kweli. 21 Maana wote wanatafuta vyao wenyewe, sivyo vya Kristo Yesu. 22 Ila mwajua sifa yake, ya kuwa ametumika pamoja nami kwa ajili ya Injili, kama mwana na baba yake. 23 Basi, natumaini kumtuma huyo mara, hapo nitakapojua yatakayonipata. 24 Nami naamini katika Bwana ya kuwa nitakuja na mimi mwenyewe hivi karibu. D. Maneno ya kipekee aliyoyatumia Paulo kuhusiana na washirika wake katika Injili 1. Mtenda kazi mwenza ( synergos ), Rum. 16:3, 7, 9, 21; 2 Kor. 8:23; Fil. 2:25; 4:3; Kol. 4:7, 10, 11, 14; Flm. 1, 24. 2. Mfungwa mwenza ( synaichmalotos ), Kol. 4:10; Flm. 23

3. Mtumwa mwenza ( syndoulos ), Kol. 1:7, 4:7 4. Askari mwenza ( systratiotes ) Flp. 2:25; Flm. 2 5. Mshirika mwenza katika kazi ( synatheleo ), Flp. 4:2-3

E. Orodha fupi ya washirika wa Paulo katika huduma (hawa waliambatana naye katika kila awamu na juhudi za kazi, watu wenye historia zinazotofautiana, karama, kazi, na wajibu mbalimbali katika njia ya huduma yake). 1. Yohana Marko (Kol. 4:10; Flm. 24)

2. Aristarko ( Kol. 4:10; Flm. 24 ) 3. Androniko na Yunia (Rum. 16:7) 4. Filemoni (Flm. 1) 5. Epafrodito (sawa na Epafra) ( Kol. 1:7; Flm. 23; Flp. 2:25 ) 6. Klementi ( Flp. 4:3 )

Made with FlippingBook Annual report maker