https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

/ 3 1 9

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

Kuwawezesha Watu kwa ajili ya Uhuru, Ustawi na Haki (muendelezo)

katika kubuni kazi zake za maendeleo ili kazi hizo ziweze kuchochea kazi kuu ya uinjilisti na upandaji makanisa badala ya kuidhoofisha. 4 Tunapaswa kushiriki katika kazi ya maendeleo ambayo inakuza uanzishaji, afya, ukuaji, na uzidishaji wa makanisa ya kienyeji miongoni mwa jamii maskini. Umahususi unaruhusu mashirika kuongeza mafunzo na rasilimali ambazo zinaweza kutengwa na kuelekezwa katika eneo maalum la kazi kubwa ya umisheni. Taasisi ya maendeleo inaweza kujihusisha katika miradi mingi mizuri na muhimu ambayo haina uhusiano wa moja kwa moja na uinjilisti na upandaji na malezi ya makanisa yanayozaliwa. Shirika la kimisheni linathamini mashirika mengi ya maendeleo ambayo yanajihusisha na aina hii ya kazi. Ingawa shirika la kimisheni litataka kuwa na ubia na shirika la maendeleo (na kuomba kwamba Mungu aongeze idadi na ufanisi wa mashirika hayo kwa kiasi kikubwa), shirika la kimisheni lenyewe litazingatia miradi ya maendeleo inayosaidia kazi ya uinjilisti, ufuasi, na uanzishaji wa makanisa ya kienyeji. Pasipo kujipambanua huku kwa umahususi, shirika la kimisheni litapoteza uwezo wake wa kukamilisha sehemu yake katika kazi pana ya Mungu. 4.1 Tamko la Dhumuni Ingawa tunatambua uhalali wa kujihusisha katika kazi za maendeleo kama mwitikio wa moja kwa moja wa kimungu kwa mahitaji ya binadamu, tunaamini kwamba tumeitwa kujikita katika kazi za maendeleo ambazo hasa zinasaidia na kuchangia katika kazi ya uinjilisti, ufuasi na upandaji makanisa. Kwa kuzingatia hili, tunapambanua msimao wetu kama ifuatavyo. Lengo la huduma za maendeleo za World Impact ni kusaidia uinjilisti, uanafunzi, na malengo ya World Impact ya upandaji makanisa kwa: • Kuonyesha Upendo wa Kristo Watu wengi waliokandamizwa wana msingi mdogo wa kuelewa upendo wa Mungu kwao na haki na huruma ambavyo ni kiini cha asili na tabia yake. Kazi ya maendeleo inaweza kutoa ushuhuda hai wa upendo wa Kristo na namna anavyojali uwepo wa haki na amani katika mitaa ya majiji. Huduma inayolenga kugusa maisha ya mtu katika ujumla wake inaweza kufanyika sanjari na utangazaji wa Injili kwa maneno, kuthibitisha uhalisia wake na kuimarisha kina cha uelewa miongoni mwa wasikilizaji wake. Shughuli ya maendeleo inaweza kufanya kazi kabla ya uinjilisti ili kuwaandaa watu kusikiliza kwa dhati maneno ya Kristo na ujumbe wake wa wokovu.

4 Tazama Kiambatisho A kupata mitazamo mbalimbali kuhusu jinsi kazi

ya maendeleo isiyotekelezwa

ipasavyo inavyoweza kuathiri vibaya kazi ya umisheni.

4. Kazi za Maendeleo ndani ya Wakala Wetu wa Umisheni

Made with FlippingBook Annual report maker