https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
3 2 0 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
Kuwawezesha Watu kwa ajili ya Uhuru, Ustawi na Haki (muendelezo)
• Kuyawezesha Makanisa Yanayochipukia Makanisa yanayochipukia mijini mara nyingi yana rasilimali chache za kimwili zinazoweza kutumika kukabiliana na mahitaji makubwa ya majiji. Taasisi ya maendeleo ya kikristo inaweza kushirikiana na wachungaji wa makanisa yaliyopandwa, ili kutoa fursa za upatikanaji wa rasilimali na programu ambazo zinaweza kukidhi mahitaji ya msingi ndani ya makusanyiko yao, kuhimiza maendeleo ya uongozi, na kusaidia makusanyiko yao kushiriki katika kuifikia jamii yao kwa namna inayohudumia mahitaji ya watu kiroho na kimwili. • Kutoa Kielelezo cha Matokeo ya Injili Hatuwezi kutegemea kuzalisha makanisa yenye nia ya dhati ya kushiriki katika kazi ambayo hawajawahi kuona ikitekelezwa kwa vitendo. Tunashiriki katika kazi ya maendeleo kwa sababu tunatarajia makanisa mapya yaliyopandwa kufanya vivyo hivyo. Tunataka kutoa mfano hai kwamba Injili lazima ichukue hatua kutoka imani hadi matokeo yaliyo dhahiri, kutoka neno hadi tendo. 4.2 Kumbusho Muhimu Kuna tahadhari hii muhimu ya kuzingatia. Hatuwezi, kwa juhudi zetu wenyewe, kuuleta Ufalme wa Mungu. Kama vile Paul Hiebert anavyotukumbusha, “Mielekeo yetu itakuwa na dosari ikiwa tutaanza kazi ya umisheni kwa shughuli za kibinadamu. Utume kimsingi sio kile tunachofanya. Ni kile ambacho Mungu anafanya” (Hiebert 1993, 158). Uinjilisti, upandaji makanisa na maendeleo, vyote hufanya kazi, kwanza kabisa, chini ya maongozi na mamlaka ya Roho wa Mungu. Kujua nini kifanyike, na jinsi tunavyopaswa kufanya, kamwe hakuamuliwi kupitia michoro ya kimkakati au mbinu ambazo mashirika yamezifanyia utafiti na kuzithibitisha. Wajibu wetu wa kwanza ni kuwa waaminifu kwa Mfalme, kusikiliza maagizo yake na kuitikia mipango yake.
Maadili ya Maendeleo
Tumeeleza kuwa: Watendakakazi wa maendeleo wanatakiwa kuwezesha watu binafsi, makanisa na makundi katika jamii kupiga hatua kuelekea uhuru, ustawi, na haki ya Ufalme wa Mungu.
5. Utangulizi
Made with FlippingBook Annual report maker