https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

3 2 2 /

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

Kuwawezesha Watu kwa ajili ya Uhuru, Ustawi na Haki (muendelezo)

• Kupata utu na heshima. • Kuwezeshwa kufanya maamuzi ya busara. • Kuwajibika kwa ajili ya maisha yao wenyewe na ya wengine.

Mchakato huu unahusisha kuwasaidia watu kuelewa na kufikia kile wanachohitaji ili kuishi kwa uhuru katika jamii kama watumishi wa Ufalme wa Mungu wanaowajibika kibiblia, wanaojiongoza, na wanaoendelea kukua. Hili linamaanisha kukuza aina ya mahusiano ambayo si ya utegemezi wala ya kujitegemea kama mtu aliye kamilika na asiyehitaji wengine, bali mahusiano ya kutegemeana kwa upendo ambayo yanaweza kuzaa ushirikiano, kuheshimiana, na kuongezeka kwa wigo wa uhuru. 6.1 Maendeleo yanawathibitishia wanadamu kuwa ni wa thamani na wa pekee machoni pa Mungu, na kuamini kwamba wamepewa uwezo wa kipekee na Mungu. Maelezo Kama viumbe walioumbwa kwa mfano wa Mungu, kila mtu bila kujali cheo au mahali alipo, anastahili hadhi na heshima. Watu wanapaswa kuthaminiwa, kutunzwa, na kufadhiliwa kwa sababu ya thamani na upekee wao wa asili mbele za Mungu. Maendeleo yenye msingi wa Kibiblia hayatawanyonya watu kwa ajili ya malengo ya kiuchumi au kuwachukulia watu kama vyombo vya kutumikishwa kufikia matokeo fulani, badala yake yatawathamini kama walengwa wakuu wa maendeleo husika, wanaostahili kupendwa na kuheshimiwa kwa sababu ya thamani waliyonayo mbele za Mungu. Ufafanuzi • Watu wanapaswa kupewa kipaumbele katika kila nyanja ya maendeleo . Maendeleo yanapaswa kuchangia katika uwezekano wa kujitosheleza, yanapaswa kuimarisha ubora wa maisha, na kuhimiza uwakili mzuri miongoni mwa wale wanaoshiriki katika programu husika. • Kuheshimiana ndio msingi wa maendeleo ya kweli . Kwa maskini, maisha katika jamii za mijini yamejaa usumbufu, shida, na aibu. Wahitaji kila siku hupitia matusi na udhalili katika jamii tajiri kwa sababu ya umaskini wao. Mara nyingi wanashutumiwa kwa utovu wa kimaadili, wanakabiliwa na urasimu kandamizi na kuhukumiwa kwamba

Made with FlippingBook Annual report maker