https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

/ 3 2 3

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

Kuwawezesha Watu kwa ajili ya Uhuru, Ustawi na Haki (muendelezo)

wanasababisha umaskini wao wenyewe kwa kukosa uwezo au kukosa motisha. Maendeleo yanapaswa kuzingatia kwa umakini mkubwa jumbe hizi zinazotolewa kwa wahitaji katika jamii zetu. Yanatambua kwamba maskini ni walengwa wa huruma, wema na habari njema za Mungu, waliochaguliwa kuwa matajiri katika imani na warithi wa Ufalme wa Mungu (Yakobo 2:5). Kupitia kazi na mahusiano mahususi, maendeleo yanatafuta kudhihirisha namna ambavyo Mungu katika haki na ukarimu wake anawapenda na kuwajali maskini. Misaada isiyotolewa kwa msingi wa heshima ya kweli inaweza kuwadhalilisha maskini kwa urahisi. Kwa hiyo, msaada unaotolewa kwa wahitaji lazima uthibitishe utu na heshima yao. Kitu chochote katika mchakato wa maendeleo ambacho kinapunguza thamani na umuhimu wa watu kwa sababu ya umaskini ni dhambi na ni chenye madhara kwa ustawi wa pande zote, wale wanaotoa msaada na wale wanaopokea. • Mahali pa kazi panapaswa kutumika kama jumuiya inayojali. Ingawa mazingira mengi ya kazi yana sifa ya kutojali utu, maendeleo ya Kikristo yanapaswa kujitahidi kuunda mfumo bora wa mahusiano baina ya walengwa na wafanyakazi. Watenda kazi wa maendeleo na wale wanaoshiriki katika mradi wa maendeleo lazima watengeneze mienendo inayokuza mazoea ya kujaliana pasipo kujalisha changamoto za mradi husika. 6.2 Maendeleo yanapaswa kuwawezesha watu kuwajibika kikamilifu kwa ajili ya maisha yao wenyewe na kujali mahitaji ya wengine . Maelezo Maendeleo yanatokea kutokana na imani kwamba kazi zote ni za heshima. Mungu ameamuru kwamba wanadamu wapate riziki zao kwa uadilifu na ubora. Agizo hili la kazi ya mtu binafsi limejikita katika amri ya awali ya Mungu waliyopewa wanadamu wakati wa uumbaji, na inaendelea na kuthibitishwa tena katika mafundisho ya mitume. Ingawa Mungu anataka kwamba watu wake wawe wakarimu kwa wenye uhitaji na wageni (2 Kor. 9), Mungu vivyo hivyo amewaamuru watu wote wafanye kazi kwa unyoofu kwa mikono yao wenyewe (1 The.4), na zaidi ameagiza kwamba wale wanaokataa kufanya kazi wanapaswa kunyimwa misaada, yaani, “ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi asile chakula” (taz. 2 The.3:10).

Made with FlippingBook Annual report maker