https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
3 2 4 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
Kuwawezesha Watu kwa ajili ya Uhuru, Ustawi na Haki (muendelezo)
Maendeleo yanakataa dhana ya kwamba kutengeneza ukwasi ni uovu kwa asili. Mtazamo kama huo ni mwepesi (hauna uzito wala mantiki) na utashindwa kusimama mbele ya wazo la kibiblia la uwakili wa Kikristo. Maendeleo yanalenga kutengeneza utele, lakini kamwe si kwa ajili ya faida ya ubinafsi au uchoyo na tamaa. Badala yake, maendeleo yanachukulia kwa uzito takwa la kibiblia kwamba tufanye kazi, si tu kukidhi mahitaji yetu wenyewe, bali ili kutokana na utele ambao Mungu anatukirimia tuweze kutumia mali na rasilimali zetu kukidhi mahitaji ya wengine, hasa wale ambao ni ndugu na dada zetu katika mwili wa Kristo (rej. Efe. 4; 2 Kor. 8; Gal. 6). Kiwango cha kibiblia ni kwamba wale walioiba kabla ya kuingia katika Ufalme wasiibe tena, bali wafanye kazi za heshima kwa utulivu na uadilifu, ili wawe na rasilimali za kutosha kukidhi mahitaji yao wenyewe, na kuwa na mali za kutosha kuwajali wengine. Maendeleo si tu kwamba yanalenga kuwaheshimu wahitaji kwa kuhakikisha kwamba wanaweza kushiriki katika haki ya msingi ya binadamu ya kufanya kazi, pia yanawapa changamoto ya kumwamini Mwenyezi Mungu kuwatimizia mahitaji yao kwa njia ya kazi za heshima zinazowawezesha kuwa wafadhili wao wenyewe na wa wengine. Ufafanuzi: • Hakuna kitu kinachoweza kumwepusha mfanyakazi, kiongozi, au mtaalamu na ulazima wa uwajibikaji binafsi na hatari zinazoweza kujitokeza kutokana na kutokuwajibika. Wafanyakazi Wakristo hawana kinga ya moja kwa moja itakayowazuia kuingia katika mazoea mabaya ya uvivu, uzembe, usimamizi mbaya, na pupa, na hawataepushwa na matokeo ya tabia na mienendo kama hiyo. • Ni lengo la msingi la maendeleo kukuza ukomavu wa kila mtu anayehusika katika mchakato na shughuli hizo. Inachukuliwa kuwa mtu anayepevuka atazidi kuwa na sifa ya maono (kujiwekea malengo, matarajio na vipaumbele vya maisha), uwajibikaji (kutenda kulingana na malengo, matarajio na vipaumbele hivyo kwa motisha, uvumilivu na uadilifu), na hekima (kuongezeka kwa ustadi, ufahamu na uwezo wa kupambanua na kufanya kile kinachofaa kwake mwenyewe na kwa wengine). Watu wanaokomaa wanapaswa kuhama kutoka katika hali ya utegemezi kuelekea uhuru, kutoka katika hali ya kutokuwa na shughuli (kukaa tu) kuelekea katika maisha yenye shughuli na wajibu, kutoka uwezo mdogo
Made with FlippingBook Annual report maker