https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

/ 3 2 5

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

Kuwawezesha Watu kwa ajili ya Uhuru, Ustawi na Haki (muendelezo)

hadi uwezo mkubwa, kutoka kwenye masilahi finyu hadi masilahi mapana, kutoka katika ubinafsi hadi uungwana (tabia ya kufikiria wengine), kutoka katika ujinga kuelekea kuelimika, kutoka katika hali ya kujikinai hadi kujikubali, kutoka katika kujitenga kuelekea kwenye tabia na mtazamo wa ushirikiano, kutoka katika kuiga kuelekea uhalisia na kutoka katika ugumu wa kimtazamo (kutotaka kubadilika) kuelekea uvumilivu na kuchukuliana (Klopfenstein 1993, 95-96). • Maamuzi yanakuwa na ufanisi zaidi yakifanyika karibu zaidi na wale walioathirika. Sera na taratibu za kitaifa zipo ili: » Kutoa mfumo wa kufanya maamuzi kwa ufanisi. » Kufafanua maadili na madhumuni ya pamoja kama taifa. » Kuhakikisha kuna haki na usawa kati ya watu na miradi katika maeneo mengi tofauti. » Kuleta uwajibikaji unaolinda uadilifu. Kukiwa na maamuzi makini ndani ya jamii maana yake kuna watu waliokomaa na ambao wana dhamira ya dhati ya kusimamia madhumuni haya ya pamoja na kuhakikisha kwamba kuna mawasiliano ya wazi baina ya watu wanaohusika. Vipengele hivi vinapokuwepo, maamuzi mengi yanapaswa kufanywa na watu wenye dhamana ya kutekeleza maamuzi hayo. Maamuzi yote lazima yazingatie muktadha wa ndani na upekee wa watu, mahusiano, na hali za mradi zilizopo. • Mishahara inapaswa kuwa ya haki. Kazi ya maendeleo inapohusisha ajira, mfanyakazi anapaswa kulipwa kwa usawa kulingana na mchango wake katika mafanikio au faida ya mradi. • Programu za mafunzo zijumuishe kufundisha juu ya umuhimu wa uwakili na utoaji. Umuhimu wa watu kutoa kwa Mungu, kwa wengine na kwa jamii yao unapaswa kuwekwa wazi katika mchakato wa maendeleo. Ni muhimu kuimarisha utambulisho wa kila mtu kama mchangiaji au mdau na kusisitiza uhusiano wa asili uliopo kati ya kupokea na kutoa (Luka 6:38).

Made with FlippingBook Annual report maker