https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
3 2 6 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
Kuwawezesha Watu kwa ajili ya Uhuru, Ustawi na Haki (muendelezo)
6.3 Kazi ya maendeleo lazima ilenge kuondoa mwelekeo wa utegemezi. Maelezo Maendeleo yanasisitiza kuwa kila mtu anapaswa kufundishwa na kuwezeshwa ili kufikia uwezo wake wa kujitegemea na kujiongoza. Kutengeneza au kulea utegemezi kunapunguza hitaji la kina la mwanadamu la kuwa muumba mwenza pamoja na Mungu katika kutumia vipawa vyetu kumheshimu, na kutafuta umuhimu na nafasi yetu ulimwenguni. Utegemezi unaweza kutokea kwa kusababishwa na upande mmoja au mwingine wa uhusiano wa kusaidia watu; mwanzilishi wa programu anaweza kujenga mtazamo na hisia za umuhimu wake mwenyewe, jambo ambalo linaweza kusababisha utegemezi, au mlengwa anaweza kukataa kwa urahisi kuendelea kukua kuelekea kutegemeana na kina. Utegemezi huchafua mchakato wa maendeleo ya kweli kwa kujenga uhusiano usiofaa ambao unaharibu jitihada na motisha binafsi ya mlengwa wa maendeleo. Ufafanuzi • Ni lazima kuwataka walengwa kuonyesha juhudi. Kanuni ya msingi ya kidole gumba ni “Usiwafanyie watu kile wanachoweza kujifanyia – hata kama ina maana kwamba mradi (au mafunzo) utaenda polepole” (Hoke na Voorhies 1989, 224). Kuwafanyia mengi kupita kiasi watu wanaosaidiwa ni kuwanyima fursa ya kujifunza kutokana na makosa yao. Utegemezi, hata unapotokana na roho ya ukarimu na huruma, bila shaka huzuia ukuaji wa wale ambao wameathiriwa nao. • Maendeleo yanapaswa kuepukana na mienendo iliyokithiri ya kuwatawala watu kimabavu kama watoto, kwa upande mmoja, na kuepukana na uendeshaji wa mambo kiholela pasipo mwongozo kwa upande mwingine . Watenda kazi wa maendeleo, kwa ufafanuzi, ni viongozi, na hawawezi kuepuka wajibu wao wa kushauri, kulea, kufundisha na kutoa mwelekeo kwa wale wanaowahudumia. Hata hivyo, kudumisha udhibiti kamili wa kufanya maamuzi hakukuzi mahusiano ya kutegemeana. Ingawa ufuatiliaji wa karibu ni muhimu katika hatua za awali za mafunzo, watenda kazi wa maendeleo lazima watambue haja ya kurekebisha mikakati na ushirikishwaji kwa kuzingatia uwezo na maendeleo endelevu ya wanafunzi. 5
5 Kwa ufahamu zaidi kuhusu mfumo wa mafunzo wa Hersey Blanchard ambao huzingatia mtindo wa uongozi kwa kuendana na uwezo na mitazamo ya wanafunzi, tazama Leadership Research (Klopfenstein, 1995)
Made with FlippingBook Annual report maker