https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
/ 3 2 7
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
Kuwawezesha Watu kwa ajili ya Uhuru, Ustawi na Haki (muendelezo)
• Miradi inapaswa kuwasaidia walengwa kuchukua udhibiti wa hatima zao wenyewe. Miradi lazima itathminiwe mara kwa mara ili kuhakikisha kwamba haiwafanyi watu kutegemea kuajiriwa kwa muda mrefu na shirika la kimishenari. Lengo ni kuwa na miradi ambayo inawawezesha watu kupata ajira kupitia biashara zilizopo au kuanzisha biashara zao wenyewe. Ukamilifu ( Shalom ) ni hali binafsi na ya kijumuiya yenye amani, utele, wema, uzima, ustawi, na mali. Ukamilifu unatokana na haki (mahusiano mazuri na Mungu na wanadamu), kweli (imani sahihi kuhusu Mungu na mwanadamu), na utakatifu (matendo mema mbele za Mungu na mwanadamu). Shalom ni zawadi ya Mungu na ishara ya uwepo wa Ufalme wake. 7.1 Maendeleo yanapaswa kutengeneza mazingira ambapo uhusiano wa ushirika unaweza kustawi. Maelezo Maendeleo yanayopelekea ukamilifu yanatambua kwamba shughuli za kibinadamu hufanyika katika jamii. Mtandao wa mahusiano unaotokea katika mazingira ya kazi (k.m. mkufunzi na mwanafunzi, mtenda kazi na mtendaka kazi mwenza, n.k.), lazima uakisi maadili yetu kama jamii ya Kikristo. Ufafanuzi • Watu si vifaa vya kutumia kutimiza malengo. Maendeleo yanatafuta, kwanza kabisa, kuwaendeleza watu. Hii itahusisha kuwaandaa (na kuwawajibisha) ili waweze kukamilisha kazi. Hata hivyo, kusudi lengwa la msingi la kazi ya maendeleo ni kukua na kustawi kwa mtu, sio kukamilika kwa kazi. • Watu wote katika mchakato wa maendeleo wanapaswa kutumikiana kana kwamba wanamtumikia Kristo mwenyewe . Andiko la Wakolosai 3:23-24 linatukumbusha kwamba kazi yetu hatimaye inaelekezwa kwa Kristo na kutunukiwa na Yeye. Miradi ya maendeleo lazima itekeleze kanuni hii. Hili linadokeza kwamba kazi yetu lazima ifanywe kwa ubora, uadilifu, bidii, upole, upendo na sifa nyingineyo yote inayohitajika kwa ajili ya utumishi ufaao kwa Mungu.
7. Kazi ya Maendeleo ya World Impact Inalenga Ustawi na Ukamilifu
Made with FlippingBook Annual report maker