https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
3 2 8 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
Kuwawezesha Watu kwa ajili ya Uhuru, Ustawi na Haki (muendelezo)
• Mienendo ya mahusiano lazima ichukuliwe kwa uzito. Mradi wa maendeleo ambao unaleta matokeo bora na kuwapa watu ujuzi wa soko, lakini una sifa ya mafarakano na kutokuelewana baina ya wafanyakazi wake haujafikia lengo lake. Mleta maendeleo lazima atafute kukuza mahusiano ya kweli mahali pa kazi.
7.2 Shughuli za maendeleo zinapaswa kuakisi kweli ya Injili. Maelezo
1 Yohana 3:18 hutuhimiza tupende si kwa maneno au ulimi tu, “bali kwa tendo na kweli.” Upendo wa Kristo si kwa “nafsi” pekee bali ni upendo kwa mtu katika ujumla wake. Shughuli za maendeleo zinapaswa kumhudumia mtu katika ujumla wake (yaani maeneo yote ya utu wake) na zitumike kama uinjilisti kwa vielelezo. Kazi ya maendeleo inatumika kama ishara ya Ufalme kwa kuwezesha watu, familia, na\au jamii kupata upendo na utunzaji wa Kristo. Hili linamaanisha kwamba watenda kazi wa maendeleo lazima wamjue Kristo kwa karibu na waweze kuakisi upendo wake kwa wengine. Ufafanuzi • Miradi ya maendeleo inaweza kulenga maendeleo ya kiakili, kimwili, kijamii au kiuchumi. Maeneo yote ya uhitaji wa mwanadamu ni muhimu kwa mtenda kazi wa maendeleo. Upendo wa mtenda kazi wa maendeleo kwa watu unapoendelea kusitawishwa kupitia matendo mema, nia yake inapaswa kuwa kwamba watu “wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni” (Mt. 5:16 ). • Watenda kazi wa maendeleo wanapaswa kuwa wanafunzi wa Kristo wanaokomaa ambao wamejiwekeza kikamilifu katika ukuaji endelevu wa kiroho. Jinsi tulivyo (utu na utambulisho wetu) ni muhimu zaidi kuliko kile tunachofanya. Ni pale tu wafanya kazi wa maendeleo wanapotafuta kwa bidii kuishi katika pendo la Kristo na kumsikiliza Roho wake, ndipo watakapoweza kuufikisha upendo wake kwa ufanisi kwa wale wanaowahudumia.
Made with FlippingBook Annual report maker