https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

/ 3 2 9

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

Kuwawezesha Watu kwa ajili ya Uhuru, Ustawi na Haki (muendelezo)

• Watenda kazi wa maendeleo lazima wapate matunzo kwa ajili ya afya na maendeleo yao ya kimwili, kiakili, kihisia na kiroho . Watenda kazi wa maendeleo wanakabiliwa na changamoto za kipekee katika kushughulikia mahitaji ya kibinadamu. Mara nyingi wanahisi shinikizo fulani kutokana na kusimama katikati, na kuguswa kwa kina na maslahi ya watu mahususi wanaowahudumia, wakati huo huo wakitakiwa kusimama na matakwa ya shirika wanaloliwakilisha (Angalia Hiebert 1989, 83). Kuchoka kwingi kimwili, kihisia au kiroho ni jambo linaloweza kuwatokea. Kwa hiyo, ni muhimu kwamba watenda kazi wa maendeleo watoe muda na umakini wa kutosha katika kudumisha afya zao ili waweze kuendelea kuhudumia ipasavyo mahitaji ya wengine. • Watenda kazi wa maendeleo wanahitaji kupewa mafunzo mahususi katika uinjilisti na ufahamu wa umisheni . Watenda kazi wa maendeleo ya Kikristo kwa kawaida wanaelewa kwamba maendeleo na uinjilisti vinapaswa kufanya kazi kwa ushirikiano, lakini mara nyingi hawana mafunzo ya kutosha ya uinjilisti (Ona Hoke na Voorhies 1989). Watenda kazi wa maendeleo pia wanahitaji kupokea mafunzo ya jumla kuhusu umisheni na usimamizi pamoja na mafunzo wanayopewa kuhusiana na kazi yao mahususi ya maendeleo (Angalia Pickett na Hawthorne 1992, D218-19) kwa kuwa kazi zao nyingi za kila siku zinahitaji uelewa wa taaluma hizi. Ukamilifu (ustawi) na utakatifu ni dhana zisizoweza kutenganishwa. Namna ambavyo kazi ya maendeleo inafanyika itakuwa na athari kubwa juu ya uwezo wake wa kuleta mabadiliko. Ili kazi ya maendeleo iweze kuchangia kuleta ukamilifu, uzima na ustawi wa watu ni lazima kuchukua tahadhari maalum kwa ajili ya kudumisha uadilifu katika maneno na matendo. Ufafanuzi • Miradi ya maendeleo inapaswa kudumisha viwango vya juu vya maadili. Ukosefu wa fedha au wafanyakazi wa kutosha na shinikizo la mahitaji ya haraka ya kibinadamu vinaweza kutushawishi «kupindisha mistari» katika 7.3 Shughuli za maendeleo zinapaswa kufanyika pasipo lawama. Maelezo

Made with FlippingBook Annual report maker