https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

3 3 0 /

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

Kuwawezesha Watu kwa ajili ya Uhuru, Ustawi na Haki (muendelezo)

namna tunavyoandaa na kusimamia miradi. Jaribu hili lazima lipingwe. Matokeo yetu hayawezi kutenganishwa kiholela na matumizi ya kanuni za uadilifu katika michakato yetu. Miradi ya maendeleo lazima iwe kielelezo kwa serikali, jamii kwa ujumla, na watu wanaohudumiwa kwa kuzingatia viwango vya juu vya maadili ya uendeshaji wa shughuli. • Miradi ya maendeleo lazima ifanye kazi ndani ya mfumo wa sifa yetu ya 501(c)(3) kama taasisi isiyo ya faida. Sheria za Jimbo na za kitaifa zinawekea mipaka mashirika yasiyo ya faida kuwa na uwezo wa kutengeneza mazingira ambapo watu binafsi wanaweza kupokea mali na rasilimali moja kwa moja kutoka kwa mashirika husika. (Hii inazuia watu binafsi ndani na nje ya shirika kutumia vibaya sifa ya taasisi isiyo ya faida kwa manufaa binafsi). Mipango inapowekwa ili kuwawezesha watu na kugawa rasilimali, watenda kazi wa maendeleo lazima wahakikishe kwamba wamejipanga kwa namna ambayo wanaangukia ndani ya miongozo ya kisheria. • Kuvutia wafadhili hakupaswi kuchochea hatia, kuzidisha mahitaji, kuahidi matokeo yasiyo ya kweli, au kudhalilisha utu wa wapokeaji wa misaada . Kuweka katika muhtasari ugumu wa mahitaji na mahusiano ya kibinadamu kuwa wito wa kuvutia wafadhili ni kazi ngumu na yenye changamoto nyingi. Lakini, ni kazi muhimu na ya lazima. Watenda kazi wa maendeleo katika uwanja huo wanapaswa kuchukua jukumu binafsi la kupeleka mahitaji na maono kwa njia sahihi kwa wale wanaohusika katika usambazaji wa nyenzo zinazochapishwa kuhusiana na mradi. Haki hutokana na kutambua kwamba vitu vyote ni vya Mungu na vinapaswa kugawanywa kulingana na sifa yake ya ukarimu na kutokuwa na upendeleo. Haki ya Kibiblia inahusu kutenda kwa usawa na kurejesha mahusiano sahihi. Inachukia ukandamizaji, ubaguzi na ukosefu wa usawa kwa sababu inaelewa kwamba matendo ya aina hiyo husababisha kutengana baina ya watu na kati ya watu na Mungu. Maendeleo ambayo yana msingi wa haki ni hatua muhimu kuelekea kurekebisha mahusiano yaliyoharibika kati ya watu binafsi, na baina ya matabaka na tamaduni ambazo zinaweza kuwa na mashaka na nia mbaya dhidi ya matabaka na tamaduni zingine. Kazi ya maendeleo inalenga kuibua na kukuza matendo sahihi na kupelekea mahusiano sahihi.

8. Kazi ya Maendeleo ya World Impact Inalenga Haki

Made with FlippingBook Annual report maker