https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

3 7 0 /

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

KIAMBATISHO CHA 42 Usomaji kuhusu Kanisa

Watu wa Mungu: Kuishi Matukio ya Ekklesia

1 Pet. 2:9-12 – Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu; 10 ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema. 11 Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho. 12 Mwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili, iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa. Utambulisho wa Wakristo kama “watu wa Mungu” unaonekana mara kadhaa katika Agano Jipya (k.m. Luka 1:17; Mdo 15:14; Tito 2:14; Ebr. 4:9; 8:10; 1 Pet. 2:9-10; Ufu. 18:4; 21:3). Lakini Paulo anatumia utambulisho huo akiwa na maana ya kipekee katika Warumi 9:25-26; 11:1-2; 15:10, na 2 Wakorintho 6:16, akiliweka kanisa la Kristo katika muktadha wa hadithi ndefu ya kushughulika kwa Mungu na watu wake wateule Israeli. “Watu wa Mungu,” usemi wa kiagano, ambao unazungumza kuhusu Mungu kuchagua na kuwaita watu fulani katika uhusiano wa maagano (Kut. 19:5; Kum. 7:6; 14:2; Zab. 135:4; Ebr. 8:10; 1 Pet. 2:9-10; Ufu. 21:3). Wao ni mpango wa neema ya Mungu na hatua kuu katika kuwaumba, kuwaita, kuwaokoa, kuwahukumu, na kuwategemeza. Na kama watu wa Mungu, wanauona uwepo wa Mungu kati yao. ~ Richard Longenecker, ed. Community Formation in the Early Church and in the Church Today. Peabody, MA: Hendrickson Publishers, 2002. uk. 75. Mahali Masomo ya Kibiblia ya Uongozi Huanzia: Kanisa kama Muktadha wa Mabadiliko ya Ulimwengu Somo la kibiblia kuhusu uongozi lazima lianze na hadithi ya kanisa lililozaliwa Siku ya Pentekoste. Neno ekklesia limetumika zaidi ya mara mia moja katika Agano Jipya. Kwa kweli, haiwezekani kuelewa mapenzi ya Mungu kwa ajili ya maisha yetu kama waamini bila kuelewa “siri hii ya ajabu ya Kristo” “kama walivyofunuliwa mitume wake watakatifu na manabii zamani hizi katika Roho” (Efe. 3:4-5).

Made with FlippingBook Annual report maker