https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

/ 3 7 1

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

Usomaji kuhusu Kanisa (muendelezo)

Zaidi ya Injili, sehemu kubwa ya Agano Jipya ni hadithi ya “makanisa ya mahali” na jinsi Mungu alivyokusudia yafanye kazi. Kweli, Yesu Kristo alikuja kuweka msingi na kujenga ekklesia yake (Mt. 16:18 ) na alipomwambia Petro, “Nitalijenga kanisa langu,” bila shaka alikuwa anafikiri kwa mapana zaidi ya kuanzisha “kanisa la mahali” katika Kaisaria ya Filipi ambapo mazungumzo haya yalifanyika (Mt. 16:13-20). . . . Kwa upande mwingine, Yesu pia alikuwa akitarajia wingi wa makanisa ya mahali ambayo yangeanzishwa katika Uyahudi na Samaria na katika Milki yote ya Kirumi – na hatimaye katika dunia yote kama tunavyoijua leo. Hadithi hii inaanza katika kitabu cha Matendo ya Mitume na inachukua kipindi muhimu katika karne ya kwanza (takriban kutoka mwaka 33 BK hadi 63 BK). Zaidi ya hayo, katika kipindi hiki, barua nyingi za Agano Jipya ziliandikwa kwa makanisa haya ya mahali – au kwa watu kama Timotheo na Tito ambao walikuwa wakisaidia kuanzisha makanisa haya.

~ Gene Getz. Elders and Leaders. Chicago: Moody, 2003. uk. 47-48.

Ulimwengu wa Kubadilisha, Ulimwengu wa Kushinda

Ikiwa kuna watu watakaobadilisha ulimwengu kuwa bora, inaweza kusemwa, wanapaswa kuwa Wakristo, sio Wakomunisti. Kwa nafsi yangu, ningesema kwamba ikiwa tungeanza kuuishi Ukristo wetu katikati ya jamii tunamoishi, basi ingekuwa sisi, kwa hakika, ambao tungebadilisha ulimwengu. Wakristo, pia, wana ulimwengu wa kubadilisha na ulimwengu wa kushinda. Ikiwa Wakristo wa karne ya kwanza wangetumia kauli mbiu, basi hizi ndio zingekuwa kauli mbiu zao. Zinaweza kuwa zetu pia. Hakuna sababu hata kidogo kwa nini zimilikiwe na Wakomunisti [ na Waislamu, na wasioamini katika Mungu, na waabudu miungu, na wana ubinadamu wa kidunia, na... ] ~ Douglas Hyde, Dedication and Leadership , uk. 32-33

Wanaoipindua Dunia Wenyewe Wamegeuzwa Ndani-Nje

Adui mkali zaidi akawa rafiki mkubwa. Mkufuru akawa mhubiri wa upendo wa Kristo. Mkono ulioandika hati ya mashtaka ya wanafunzi wa Kristo alipowaleta mbele ya mahakimu na kuwaweka gerezani sasa uliandika nyaraka za upendo wa

Made with FlippingBook Annual report maker