https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
/ 3 7 7
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
KIAMBATISHO CHA 47 Mungu Wetu Asimame!
Wito wa Dhati wa Maombi Endelevu kwa ajili ya Uamsho Wenye Nguvu wa Kiroho na Uendelezaji Wenye Nguvu wa Ufalme katika Miji ya Marekani. Mch. Dr. Don L. Davis, Januari 1, 2003 Imeandikwa kwa heshima ya wale wote ambao kwa miaka hii mingi, kwa imani na kujidhabihu, walikataa kumwachilia Bwana hadi alipowabariki kwa niaba ya watu maskini katika miji. Ni kichwa kirefu kama nini cha insha fupi! Hii ni heshima yangu kwa kazi ya ajabu iliyoandikwa na mchungaji na mwanazuoni Jonathan Edwards, kiongozi katika Uamsho huko kaskazini-mashariki katika karne ya 18, aliyeandika kuhusu hitaji la maombezi ili kuibua harakati mpya kwa ajili ya Mungu. Kichwa cha awali cha andiko lake kilikuwa kirefu vilevile: “Jaribio la Unyenyekevu la Kuendeleza Makubaliano ya Wazi na Muungano Unaoonekana wa Watu wa Mungu, katika Maombi Yasiyo ya Kawaida, kwa Ajili ya Uamsho wa Dini na Kusonga Mbele kwa Ufalme wa Kristo Duniani.” Edwards aliandika trakti yake ndogo mwaka 1746 baada ya kupitia vipindi viwili vya ajabu vya Roho wa Mungu, miaka ya 1734-35 na 1740-42 mtawalia. Kipeperushi cha Edwards kilionyesha imani yake ya kina kwamba ikiwa watu wa Mungu wangeomba kwa bidii, kwa kina na kwa nguvu kwa ajili ya uamsho, Mungu angeachilia nguvu za Roho wake katika jamii. Matembeleo haya ya ajabu yangesababisha watu wengi kutubu na kumwamini Kristo kama Bwana, na yangeanzisha “uamsho wa dini” ulimwenguni pote na “kusonga mbele kwa Ufalme duniani.” Wakristo wote waaminifu, kwa mujibu wa Edwards, wana wajibu chanya wa kuliombea hili. Baada ya kuelezea hoja zake hasa kutokana na tafakuri yake ya kina na ufafanuzi wake makini wa Zekaria 8:18-23 (miongoni mwa maandiko mengine), Edwards alitaka kutilia mkazo “ombi lake la unyenyekevu” kwa ajili ya harakati za maombi thabiti na zenye utaratibu mzuri zaidi ili kumsihi Mungu kutembelea watu wake. Yeye hakuwa kiongozi wa kwanza au pekee wa Kikristo wa wakati huo ambaye alikuwa akitoa wito wa “maombi yasiyo ya kawaida.” Kusema ukweli, kuna “Ukumbusho” uliokuwa umekwisha andikwa na wahudumu fulani wa Scotland ambao walisambaza mawazo yao wakati huo huo alipoandika trakti yake. Ukumbusho huu ulikuwa umesambazwa katika makanisa mengi yanayozungumza Kiingereza, lakini hasa Uingereza. Ulitoa wito wa msisitizo mpya wa “maombi yasiyo ya kawaida” katika nyakati fulani, ratiba ambayo Edwards mwenyewe aliiunga mkono, hasa kwa habari ya “Jumamosi jioni, Jumapili asubuhi na Jumanne ya kwanza ya kila robo, kwa kipindi cha kwanza cha miaka saba.”
Made with FlippingBook Annual report maker