https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
3 7 8 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
Mungu Wetu Asimame! (muendelezo)
Ingawa historia hairekodi kipindi kingine kilichoenea cha kufanywa upya katika ulimwengu unaozungumza Kiingereza hadi miaka ya 1770 (kikifuatiwa na kingine miaka ya 1790), trakti ndogo ya Edwards imechunguzwa na kusomwa na wanafunzi wengi pamoja na makusanyiko mengi ya watu wanaotamani kuona mtembeo mpya na wenye nguvu wa Mungu juu ya Kanisa na katika ulimwengu. Ninapoandika asubuhi ya leo, ninatambua kwamba kwa sasa tuko mbali sana na wakati mwingi umepita tangu ziwepo jamii za Kiingereza na Kiskoti za karne ya 18 ambamo Edwards aliandika andiko lake juu ya “uamsho wa dini.” Ninapoandika mawazo yangu juu ya mada hii kutokea nyumbani kwangu hapa katika miji ya Marekani, ninafahamu kwamba tunapoingia katika milenia mpya na mwanzo wa mwaka mpya, tumerithi ulimwengu hatari zaidi, mgumu zaidi, na wa kutisha kuliko ulimwengu wa kina Edwards na wenzake huko Scotland na Uingereza. Zaidi ya watu bilioni sita wanaishi katika sayari inayolemewa na uchafuzi wa mazingira na ongezeko la watu. Tunasimama ukingoni mwa vita, huku ripoti za vitisho vya kigaidi na mizozo ya kikabila zikivuma kupitia mawimbi yetu. Mamilioni ya watu wanaishi na utapiamlo na ufukara, na idadi kubwa ya watu wanaishi katika hali ya kukata tamaa na kukosa tumaini katika ulimwengu ambao kimsingi hauna haki na haumchi Mungu. Kama kuliwahi kuwa na wakati wa kufanya upya wito wa unyenyekevu na wa dhati kwa ajili ya “maombi yasiyo ya kawaida” kwa niaba ya jamii ya watu, wakati, na majira, ni sasa. Kati ya maeneo yote magumu na yenye shida kuyafikia leo duniani, miji ya Marekani bila shaka ni mojawapo ya miji migumu zaidi. Viwango vya juu vya umaskini, vurugu, kukata tamaa, na kupoteza tumaini vinafanya juhudi za kawaida kuwa pungufu na kuonekana hazifai kabisa. Ninaamini kwamba ikiwa tu Mungu atazuru, ikiwa Bwana atainuka na kuwatawanya adui zake, kama ilivyonenwa katika Zaburi 68, ndipo uhuru, ustawi, na haki vitatawala, ndani ya watu wa Mungu waishio katika majiji yetu na kupitia kwao neema hiyo itawafikia na wale walio katika uhitaji mkubwa wa neema na riziki za Mungu. Trakti hii, kama ile ya Edwards, inawakilisha jaribio lingine la unyenyekevu la kuwahamasisha waamini kumlilia Mungu mchana na usiku kwa niaba ya Kanisa lililolala na wale wanaoteseka na kufa bila Kristo. Kilio cha moyo hapa, hata hivyo, kinalenga miji ya Marekani. Hili linawakilisha ombi la dhati la kuita nguvu, jeshi la waombezi wanaomcha Mungu na wanaopatikana ambao watajitolea kumlingana Mungu katika maombi endelevu kwa ajili ya kupenya kwa nguvu za Mungu, kwa ajili ya kuamka kiroho kwa watu wake na kuendeleza Ufalme wake katika Miji.
Made with FlippingBook Annual report maker