https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

3 8 0 /

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

Mungu Wetu Asimame! (muendelezo)

ambayo yanaweza kufanywa kwa starehe na kwa urahisi “kila robo nyingine” na kadhalika. Badala yake, tunachosisitiza hapa ni mtazamo mapya kabisa wa kujiona sisi wenyewe na majiji yetu kama tusio na nguvu wala hatima ikiwa Bwana hatoingilia kati. Tunaomba hapa kwa ajili ya mwelekeo mpya wa maisha yetu kuelekea katika mkazo mpya wa maombi kwa Mungu kutokana na kugundua na kuthibitisha kwa upya kwamba ni Mungu pekee anayeweza kubadilisha miji ya Marekani. Kusema ukweli, imani yangu ya dhati kabisa inaendelea kuwa kwamba miji ya Marekani haiwezi kuvunwa kwa Kristo pasipo kutembelewa upya na Mungu. Takriban watu milioni sitini wanaishi katika jamii zetu maskini zaidi za mijini, huku zaidi ya 90% ya wakazi hawa wakidai kutokuwa na ujuzi au uhusiano na Mungu katika Yesu Kristo. Jamii hizi zinazoteswa zimetiwa makovu makubwa na kuharibiwa na ghasia, zimepuuzwa sana na kunyonywa kiuchumi, na zinakabiliwa na matatizo makubwa na ya kutisha yanayohusiana na afya. Miji yetu ya Marekani ni hatari katika maeneo kadha wa kadha na tofauti, na bado hatari inaendelea kuongezeka kutokana na idadi ya wahamiaji na tofauti za kikabila na rangi zinazosumbua akili. Labda shida kubwa zaidi ya zote, miji ya Marekani inakabiliwa na kuvunjika moyo na kukata tamaa kwa kule kuamini kwamba maisha hayana maana na kushindwa kwa mifumo ya kijamii; kila mtu anaonekana kuishi kwa hofu na woga, akiwa na hisia kali ya kukosa tumaini. Cha kusikitisha ni kwamba, unaweza hata kupata Wakristo wanaonukuu Maandiko wakitabiri pamoja na mapambio ya waliberali na wahafidhina ambao wanaomboleza msiba na kuangamia kwa majiji. Wataalamu wengine wa umisheni wanadai kwamba Marekani tayari imekwisha kuvunwa, na kwamba makanisa ya kikabila na ya mijini yanaweza kumalizia kazi katika miji ya Marekani. Wengine hata wanatilia shaka ikiwa majiji yanafaa kuvunwa, wakitoa hukumu ya kusikitisha kwamba wale wanaoteseka huko wanavuna tu kile walichopanda kimakusudi. Katika mazingira ya umaskini wa kimwili kama huo, familia zilizovunjika, shule zisizo na viwango, huduma duni za kijamii, na giza la kiroho kwa ujumla, wengi hawatarajii jambo la maana kutoka katika majiji. Maneno na mwenendo wao hudhihirisha uhalisia wa imani yao ndani kabisa ya mioyo yao: wanashangaa kweli ikiwa kuna kitu chochote kizuri kinachoweza kutokea katika miji yetu, ambayo bila shaka ni kama Nazareti zetu za karne ya 21. Licha ya viwango hivyo vya chini vya imani, ninaamini kwamba maneno ya Biblia ni sahihi inaposema kwamba hakuna lisilowezekana kwa Mungu (Luka 1:37). Hakuna lililo gumu kwa Mungu (Yer. 32:26), na yeye kwa uwezo wake anaweza kuwagusa na kuwabadilisha wakaazi wa miji! Daima tuko tayari na tunatumaini

Made with FlippingBook Annual report maker