https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
/ 3 8 1
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
Mungu Wetu Asimame! (muendelezo)
kwamba Mungu atawatembelea watu wake mijini, na kwamba kupitia kumiminwa kwa Roho wake tunaweza kuona mlipuko wa harakati za uamsho wa kiroho na kufanya wanafunzi wa tamaduni mchanganyiko kati ya watu maskini wa mijini. Harakati hizi hazitatokea kwa sababu ya werevu na bidii ya mwanadamu, lakini kupitia nyakati za kuburudishwa kutoka kwa Bwana (Mdo. 3:19). Tunasadikishwa kwamba kuvunwa kwa miji ya Marekani kunawezekana tu kwa mpenyo wa uweza wa Mungu katika njia na viwango vya ajabu. Ni Mungu kuwatembelea watu wake kupitia uwepo na nguvu za Roho Mtakatifu wake ndiko kunaweza kusababisha aina mpya na yenye ufanisi na matunda ya kufikia miji ambayo inaweza kuleta mabadiliko kwa maelfu ya maisha kupitia nguvu za Kristo. Kama waamini na askari wenzenu katika ushuhuda wa Ufalme, tunatoa wito kwa waamini kila mahali wanaoguswa na hitaji la miji ya Marekani kuungana nasi katika harakati za Mungu Wetu Asimame! Tunawaita wote wanaowapenda wale wakaao mijini kwenye njia mpya ya kuishi – chini ya ubwana mkuu wa Yesu Kristo. Tunawaita wote wanaolipenda Kanisa la mjini kwenye njia mpya ya kumtafuta Mungu – kwa bidii na shauku, watu ambao watamlilia Bwana mchana na usiku. Tukiwa tumejawa na roho ya shauku na unyenyekevu, ni lazima tuutafute uso wa Bwana kwa bidii katika maombezi, na kufanya hivyo kimkakati, kwa utaratibu na ufanisi. Nisikilize vizuri, shujaa mwenzangu katika Kristo! Harakati za Mungu Wetu Asimame! kama vile ndugu Edwards alivyofanya huko Uingereza, ni jaribio lingine la unyenyekevu la kuwasihi, kila mwanafunzi wa Kristo anayeguswa na watu maskini katika miji ya Marekani, mjiunge nasi katika maombi ya kudumu ili Mungu ainuke na kuwatawanya adui zake. Tunatafuta kuwezesha na kutoa changamoto kwa watu binafsi, vikundi vidogo, makusanyiko yote katika maeneo mbalimbali kukutana mara kwa mara katika nyumba zao, makanisani, katika biashara, shuleni—popote ambapo Bwana anawaongoza kuomba – kumsihi Mungu atembelee miji yetu.
Mpango wa Namna ya Kumtafuta Mungu na Kusihi Kibali Chake
Kipaumbele chetu cha juu zaidi katika maombezi, kama andiko la Zekaria linavyosema, ni kwamba lengo letu kuu liwe “kumtafuta Bwana” kuliko maombi mengine yoyote. Hatupaswi kuweka kutafuta baraka au fadhili zake kuwa mbadala wa kumtafuta Yeye kwanza. Mungu Wetu Asimame! kimsingi ni wito kwa wanafunzi wa Yesu kujitolea tena kwa kiwango kipya cha hali ya kiroho, uwazi, na kupondeka mbele za Mungu ambayo itasababisha Mungu kutembelea
Made with FlippingBook Annual report maker