https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
3 8 2 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
Mungu Wetu Asimame! (muendelezo)
watu wake kwa namna ya pekee mijini. Wito huu wa dhati kwa ajili ya maombi endelevu umejikita katika ukweli kwamba hatuwezi wenyewe bila Bwana. Wito huu haujakusudiwa kuwa kama aina fulani ya kazi ambapo tunaweza kudai kupewa kibali cha Mungu, wala hatujaribu kumhonga Mungu kwa kuwa na msimu mfupi na uliokadiriwa wa unyenyekevu mbele zake. Badala yake, tamaa yetu ni kubadilishwa na Mungu kabisa. Tunatamani kwamba Mungu atembelee majiji, lakini ikiwa atatutembelea pia! Tunatamani mabadiliko ya miji na majiji, lakini tunatamani hata zaidi kwamba uamsho huu uanze na mabadiliko ya maisha yetu chini ya ubwana wa Yesu Kristo! Tuna njaa ya uwepo wake zaidi – upendo zaidi, nguvu zaidi, uwepo wa Bwana zaidi. Tunatamani kwanza kabisa kudumu katika maombi kwa kina, kwa uwazi, kwa unyenyekevu, tukimtafuta Bwana mwenyewe, kumjua kwa undani na kumtukuza katika maisha yetu – kupitia maisha yetu na utu wetu. Zaidi ya yote, shauku ya vuguvugu la Mungu Wetu Asimame! ni kwamba waamini wa mijini wamtafute Bwana kwanza – kumjua, kumwona, na kushuhudia kwa namna mpya nguvu na baraka zake maishani mwetu kama wanafunzi wake. Hii ina maana kwamba kama vuguvugu, harakati za Mungu Wetu Asimame! zinaelewa uhalali wa vipaumbele vilivyoelezwa katika Maandiko yote, na hasa katika andiko la Zekaria sura ya 8. Mstari wa 22 unaonyesha hili wazi: “Naam, watu wa kabila nyingi na mataifa hodari watakuja Yerusalemu kumtafuta Bwana wa majeshi, na kuomba fadhili za Bwana.” Tunakikaribia kwa ujasiri kiti cha enzi cha neema ya Mungu, si Yerusalemu ya kidunia, bali Mlima Sayuni wa juu, ambako Mungu wetu mwenye neema anakaa. Waebrania sura ya 12:22-24 inasisitiza hili: “Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi, 23 mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika, 24 na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili.” Hakika, kipaumbele chetu cha kwanza, zaidi ya yote, ni kuutafuta uso wa Bwana kwa mioyo yetu yote, kumjua, na kumfanya Yeye peke yake kuwa lengo na kusudi letu katika maombi.
Kuabudu, Kukubalika, na Kupatikana
Maelezo yafuatayo ya vipengele mbalimbali vya kipindi cha maombi cha Mungu Wetu Asimame! yanawakilisha muhtasari wa haraka wa aina ya maombi na njia ya kumkaribia Mungu tunayotafuta kuwa nayo. Hatutafuti kuleta muundo wa
Made with FlippingBook Annual report maker