https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

/ 3 8 3

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

Mungu Wetu Asimame! (muendelezo)

lazima katika mapendekezo yetu, lakini tunatoa yafuatayo kama aina ya kielelezo, mfano au ramani ya kutuongoza pamoja tunapotafuta uso na udhihirisho wa Mungu. Tunatumahi vipengele hivi vinaweza kutupa mwelekeo wa kivitendo tunapokusanyika katika nyumba zetu na makanisani kwa ajili ya maombi endelevu kwa Bwana. Kwa kuanzia, tunaanza vipindi vyetu vya maombi kwa kumwabudu Bwana. Hii ni awamu ya Kuabudu ya matamasha yetu ya maombi. Mikusanyiko ya Mungu wetu Ainuke! inawatia moyo wahudhuriaji kuanza tamasha lenu na kipindi cha maombi ya kina pamoja na kipindi cha kuabudu na kusifu, kuimba na kumwinua Bwana, ambapo tunamwadhimisha na kumfurahia Bwana kwa kupiga makofi, vifijo vya furaha, na sifa za kutoka moyoni. Ni lazima tumshukuru Mungu kwa kazi yake ya neema kwa ajili yetu katika Kristo, na kushukuru kwa nafasi ya kuja mbele zake kwa njia ya damu ya Kristo. Zaidi ya yote (mahitaji, dua na matamanio yote), Mungu wetu anastahili kuabudiwa na kusujudiwa kwa jinsi alivyo! Kisha, tunahamia katika sehemu ya Kukubalika (toba) ya kipindi chetu cha maombi. Baada ya kukiri utukufu na ukuu wa Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, basi tunatumia muda wa kutosha kukiri makosa na uhitaji wetu mbele ya mkono wake wenye nguvu. Ebu tujifunze kuinama mbele za Bwana kwa ukiri wa unyenyekevu wa dhambi zetu, na kukubali kwamba hatuna uwezo, hatuna nguvu, na hatuna ulinzi bila usimamizi, upaji, na neema yake. Tusifiche dhambi zetu bali tuungame kwa wepesi. Tusije tukajidhania kuwa hatuna hatia wala kujivunia ukamilifu wetu wa kiroho (Lk. 18:9-14), bali tunyenyekee kwa uaminifu mbele za Bwana ili apate kutuinua (1 Pet. 5:6). Mungu kwa kweli huwapinga wale wenye kiburi (yaani, wale wanaojifanya kuwa wanajitosheleza katika hekima, nguvu, na uwezo wao wenyewe na si wahitaji) na huwapa neema yake wanyenyekevu (yaani, wale walio tayari kukiri kutokuwa na uwezo na kukata tamaa kwao mbele za Bwana, Yakobo 4:6). Hatimaye, sehemu ya “ Kupatikana ” ya tamasha letu inazingatia kujitoa kwetu kwa furaha kwa maisha yetu mbele za Bwana kwa ajili ya utukufu na makusudi yake. Wakati huo, tunajiweka wakfu upya kwa Bwana, tukithibitisha kifo chetu pamoja na Kristo na kufufuka kwetu katika maisha mapya kwa utukufu na sifa za Mungu (Rum. 6:1-4). Tunasalimisha vyote tulivyo na kila kitu tulicho nacho kwa Yesu Kristo ili apate kututenga kwa ajili ya shauri lake na maslahi yake, na kwamba apate kufurahishwa kama matokeo ya yote tunayofanyika, tunayofanya, na kufanikisha katika maisha yetu. Paulo anaeleza jambo hili anapowaambia Wakorintho katika 2 Kor. 5:9-10 “Kwa hiyo, tena, ikiwa tupo hapa, au ikiwa hatupo hapa, twajitahidi kumpendeza yeye. 10 Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti

Made with FlippingBook Annual report maker