https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
3 8 4 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
Mungu Wetu Asimame! (muendelezo)
cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya.” Nia na lengo letu la wazi ni kumpendeza Bwana! Kwa hiyo, katika sala, tusiweke tegemeo letu katika hekima au nguvu zetu za kimwili. Zaidi ya hayo, tuache kutegemea kabisa hekima ya kidunia, na tujitoe wakfu kikamilifu katika kujitolea kuwa na kufanya chochote ambacho Bwana Yesu anataka, hata kama ni cha kutugharimu au kigumu kiasi gani. Katika maombi ya unyenyekevu, kwa maelfu yetu tupige magoti yetu kwa Bwana katika kujisalimisha kwa kweli, tukimpa Roho wake haki na nafasi atuongoze popote anapoamua, kwa njia yoyote na kwa kusudi lolote awezalo kutuelekeza kwa ustadi (Yohana 3:8). Ni aina hii tu ya kupatikana kwetu mbele za Mungu kwa kiasi kikubwa, bila masharti, itakayomruhusu kututumia wakati atakapomimina Roho wake Mtakatifu juu ya miji ya Marekani! Bila kujali maneno yanayotumiwa katika fasihi ya kitaalamu kwa habari ya kutembelewa na Mungu katika uamsho au kuamka (k.m., uamsho, upya, kuburudishwa, ufunuo, n.k.), ukweli unaozungumzwa ndani ya nyenzo hizi zote kwa ujumla unarejelea jambo hilo hilo. Ukweli gani huu? Zaidi ya mengine yote, nyenzo hizi zote zinaelekeza kwenye hitaji la uwepo wa Mungu kama jambo kuu katika kufanywa upya na kusimama kama mashahidi wa Ufalme. Miji ya Marekani leo hasa inahitaji kutembelewa upya na Bwana. Mungu lazima asimame katika miji; lazima ashuke na kuwatawanya adui zake, na kumimina tena wema na fadhili zake. Roho Mtakatifu lazima amwagike juu ya majiji ili yaweze kweli kuvunwa kwa ajili ya Kristo. Pasipo uwepo wa Mungu mwenyewe katika majiji yetu, hakuna chochote jijini kitakachotosha. Hakuna masuluhisho mengine yenye uwezekano wa kuleta mabadiliko ya kudumu au ya kina katika maisha ya mamilioni ya watu wanaoteseka katika majiji. Hakuna jibu la kawaida linaloweza kugusa maisha ya wengi; hakuna masuluhisho ya serikali, uhisani wa kijamii, mageuzi ya kisiasa au ya kisheria, au kuajiri polisi zaidi wa kupambana na uhalifu au kuondoa aina mbalimbali za “mambo machafu” katika vitongoji maskini kutashinda nguvu na utawala wa giza ambao unazisumbua jamii zetu za mijini. Mahitaji ya kiroho lazima yatimizwe kwa kutumia nyenzo na rasilimali za kiroho. Kadhalika, kanisa dhaifu lenye utapiamlo, uvivu, na akili ya kidunia halitafanikisha kazi hii ya kuwaweka huru wafungwa. Kama waamini, tumeitwa tuwe hodari katika Kwa Uamsho wa Kiroho Wenye Nguvu
Made with FlippingBook Annual report maker