https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

/ 3 8 5

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

Mungu Wetu Asimame! (muendelezo)

Bwana na katika uweza wa nguvu zake (Efe. 6:10-12). Yesu ni shujaa wa Mungu ambaye atakamilisha ushindi wa Mungu duniani wakati wa Ujio wake wa Pili (rej. Ufunuo 19:8-). Ni pale tu Kristo atakapojifunua, yeye pekee awezaye kumfunga “mtu mwenye nguvu ambaye ni ibilisi” na kuwaweka huru mateka wake (rej. Mt. 12:25 30), ndipo tunapoweza kuona uhuru, ukamilifu, na haki ya Ufalme vikiwakomboa waliopotea wakaao katika miji na majiji. Omba Neema ya Bwana kwa ajili ya Matatizo ya Ulimwengu na ya Mahali Ulipo Kwa sababu tunaamini kwa moyo wote kwamba Mungu anapenda watu wote kila mahali, tunakazia juhudi zetu za maombi tukitilia mkazo masuala ya kimataifa na ya ndani . Mzigo wa “kimataifa” unamaanisha kwamba kila wakati tunapokusanyika hatuombei tu mahitaji ya miji ya ndani ya Marekani pekee, bali tunaomba pia kwa ajili ya mahitaji ya ulimwengu mzima, miji, mataifa, na makundi ya watu ambamo Kanisa la Yesu Kristo linabeba ushuhuda, pamoja na wale wote ambao bado hawajasikia Injili ya Bwana iokoayo. Tunaamini katika Kanuni ya Imani ya Nikea, kwamba kuna Kanisa moja tu, takatifu, katoliki (la ulimwengu mzima) na la kitume, na kwamba kile kinachowahusu Wakristo popote pale kinapaswa kuwahusu Wakristo kila mahali. Pia tunaamini katika Agizo Kuu la Yesu, kwamba Kanisa limeitwa katika milenia hizi mbili kushuhudia Ufalme wa Mungu katika Yesu Kristo kwa kila kundi la watu duniani. Kwa hiyo tunaomba kwa ajili ya Uamsho wa Kanisa la Yesu Kristo kila mahali, tukimsihi Mwenyezi Mungu atende kwa ajili ya makusanyiko ya waamini popote wakusanyikapo, katika mataifa na mabara mengine, wote tukiwa na nia ya kwamba Mungu ajitukuze mwenyewe katikati ya watu wake popote watakapokusanyika. Mzigo wa “ndani” unahitaji usikivu na maombi yetu kwa uwiano na usawa. Kwa neno ndani tunamaanisha kanisa fulani tunaloshiriki, makanisa katika dhehebu letu na jamii inayotuzunguka, na kanisa katika eneo au ukanda wetu. Kila eneo la kanisa lina masuala, changamoto na mahangaiko yake mahususi na ya kipekee, na maombezi yetu yanatambua masuala haya mahususi katika jamii yetu ya Kanisa. Tunaomba upendeleo wa Bwana kwa niaba ya kusanyiko letu la kanisa la mtaa, na makusanyiko katika jiji letu, mkoa na ukanda.

Made with FlippingBook Annual report maker