https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

3 8 6 /

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

Mungu Wetu Asimame! (muendelezo)

Kwa hiyo tunaanza maombezi yetu kwa kusihi, dua, na sala maalum zinazotolewa kwa niaba ya watu wa Mungu kwa ajili ya Uamsho wa kiroho wenye nguvu. Tuombe kwa ajili ya Kanisa ulimwenguni (na sehemu mbalimbali za dunia) kwamba waamini waburudishwe kwa kumiminwa mara kwa mara na kwa nguvu na madhihirisho ya uwepo wa Roho Mtakatifu katikati ya watu wake. Tuombe kwamba Mungu aambatanishe umwagiko huu endelevu na ishara na maajabu ambayo yanaelekeza fahamu na uangalifu wetu kwenye utukufu na utawala wake, na kwamba hali ya kiroho ya makanisa ifanywe upya ili kutii Amri Kuu kwa nguvu zote. Tuombe kwamba makanisa duniani kote na ndani ya nchi yampende Mungu kwa mioyo yao yote, na jirani zao kama nafsi zao wenyewe. Tuombe kwa ajili ya upatanisho, umoja, na urejesho wa mahusiano kati ya waamini duniani kote, na tumwombe Mungu aumbe roho mpya ya umoja na makubaliano kuhusu maendeleo ya Ufalme wa Mungu katika makanisa yetu. Katika suala hili, na tuombe ugunduzi mpya wa kimapinduzi wa ubwana wa Yesu Kristo katika makanisa yetu, kwa udhihirisho wenye kuburudisha wa unyenyekevu, toba, mioyo iliyopondeka na upendo miongoni mwa washirika, yote kwa ajili ya utukufu wa Mungu. Na tufanye maombi haya na mengine yenye nia hii moja kwa niaba ya watu wa Mungu, kwa bidii na kwa akili iwezekanavyo, tukifanya maombi mahususi ya kumsihi Mungu kwa ajili ya uamsho na upya wa watu wake duniani kote, na hasa katika miji ya Marekani. Kwa moyo uliowazi na uliojaa imani, basi, tuombee makanisa katika miji ya Marekani. Tuyaombee ulinzi dhidi ya vurugu na ufisadi unaowazunguka. Tuombe kwa ajili ya ujasiri na ukweli wanapomshuhudia Kristo aliyefufuka katika kazi zao za haki, upendo na uinjilisti. Tuombe kwa ajili ya hisia mpya ya furaha na nguvu katika Roho Mtakatifu, ufunuo mkubwa zaidi unaotokana na Neno la Mungu, uzoefu mpya wa nguvu ya utakaso ya damu ya Kristo, na mtembeo wa Mungu uliojaa neema, uweza na utajiri. Tuombe kwa ajili ya roho ya utulivu na amani, kufungwa kwa adui, ili Injili iweze kusonga mbele. Pia, tuombe kwa ajili ya roho mpya ya sifa, kuabudu, na shangwe katika makanisa ya mijini, na kwa ajili ya ubunifu mpya, furaha na nderemo katika uwepo wa Mungu. Tuombe kwa ajili ya kiwango kipya cha uwazi na umoja miongoni mwa waamini, na upendo wa ndani zaidi na zaidi na kumcha Mungu katika makanisa. Tuombee viwango vipya vya heshima na hofu ya Mungu miongoni mwa watu wake, na vuguvugu jipya la ibada, maombi na sherehe katika jumuiya. Tusiishie hapa. Tuombe kwamba Mungu avunje ngome za adui kwenye akili na mioyo ya wale wanaoishi katika miji ya Marekani (2 Kor. 4:4). Tumwombe

Made with FlippingBook Annual report maker