https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

/ 3 8 7

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

Mungu Wetu Asimame! (muendelezo)

Roho Mtakatifu azuie mipango ya shetani ya udanganyifu na kukatisha tamaa, na kwamba milango mipya ifunguliwe kwa ajili ya kutangazwa na kuenea kwa Neno la Mungu katika ngazi zote. Omba ili Kanisa litoe ushuhuda kwa maneno na matendo kwa ujasiri juu ya utawala wa Mungu katika Yesu Kristo, kwamba waamini mmoja mmoja, vijana, wa umri wa kati na wazee, waonyeshe katika maisha yao viwango vipya vya upendo na nguvu za Bwana katika familia zao, kwa marafiki, na katika mitandao yao ya mahusiano. Ombea viwango vipya vya kupendezwa, udadisi, na ufahamu katika mambo ya kiroho miongoni mwa wote wanaoishi mijini, lakini hasa viwango vipya vya ukweli na nguvu miongoni mwa waamini katika majiji. Omba ili shetani asiweze kuzuia fursa ambazo Mungu anazifungua kwa ajili ya watu kumjia Kristo katika ngazi zote za jamii na ujirani. Omba kwamba Mungu ajae na kufurika katika miji na majiji, ili miji na majiji yote ya Marekani yaweze kuamshwa na kugundua upya namna yanavyomwitaji Mungu katika Yesu Kristo! Tunapojinyenyekeza katika maombi kwa ajili ya Uamsho wa kiroho wenye nguvu katikati ya watu wa Mungu, inatupasa kumwomba Mungu vile vile ili awatembelee waliopotea, watu na maeneo ambayo bado hayajapata kuijua huruma ya Mungu kupitia Bwana Yesu Kristo. Kila wakati tunapokusanyika katika matamasha ya maombi, tunapaswa kumlilia Mungu ili atembee katika majiji yetu, ili miji na majiji yashuhudie Kuenea kwa Ufalme kwa namna yenye nguvu na endelevu. Mojawapo ya sifa kuu za harakati hizi za Mungu Wetu Asimame! ni kuona Mungu akitembea katika maana hii yenye pande mbili: kuziamsha jamii za mijini kupitia utukufu na uweza wake katika Kanisa lililofanywa upya na kuhuishwa, na kuona utawala wake ukisonga mbele miongoni mwa wale wanaoishi mijini na bado hawajasikia wala kuitikia habari za upendo wa Mungu katika Kristo. Kwa hivyo, katika kipengele chetu cha tamasha letu kinachohusiana na Uenezi na tuombe kwa ajili ya mpenyo wa nguvu za Roho juu ya adui, duniani kote, katika mazingira mahususi ambayo tunayajua, na ndani ya nchi, katika maeneo mahususi katika eneo letu na ukanda wetu. Tuombe kwamba Roho Mtakatifu amimine nguvu zake juu ya watumishi wa Mungu, timu, mashirika, na makanisa ambayo yanavuna roho, kufanya wanafunzi, na kuanzisha makanisa duniani kote. Katika maeneo ambayo hayaruhusu ushuhuda wa Injili ya Kikristo, tuombe kwamba Kwa ajili ya Kueneza Ufalme

Made with FlippingBook Annual report maker