https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

3 8 8 /

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

Mungu Wetu Asimame! (muendelezo)

Mungu aguse mioyo ya viongozi wa serikali na wa kidini, waweze kuwaruhusu waamini kuingia katika jamii zao ili kuitangaza Injili ya Ufalme kwa uhuru. Ombeni pia ili Roho Mtakatifu awape waliopotea mafunuo ya ajabu ya Mungu na ya Kristo, kwamba awape ndoto na maono, kama alivyofanya kwa watu wa Makedonia (taz. Mdo. 16:9). Mafunuo haya yataweza kuweka msingi wa kiroho wa uwasilishaji wa Neno la Mungu kuhusu Kristo katika maeneo magumu na ya kikaidi. Omba kwamba makanisa, madhehebu, na mashirika ya kimisheni yaliyohuishwa yatengeneze ushirikiano mpya wa kimkakati ambao utaongoza kwenye misukumo na mienendo muhimu ya kiinjilisti katika maeneo magumu zaidi na ambayo hayajafikiwa kabisa ya mataifa ya ng’ambo na hapa nyumbani. Zaidi ya hayo, omba kwamba uamsho wa Kanisa duniani kote na ndani ya nchi uelekeze kwenye juhudi za jumla za kuhamasisha washirika wa Kanisa kwa ajili ya maendeleo mapya ya utume. Tuombe kwamba Mungu awachochee watu binafsi, wachungaji, watenda kazi Wakristo, na waamini wa kawaida kutoka katika kila kusanyiko kuombea ndugu na marafiki ambao hawajaokoka, wapate mafunzo ya kushirikisha wengine imani yao kwa ufanisi, na kujitolea kuzidisha utoaji na michango yao katika kutimiza Agizo Kuu. Omba kwamba waseja na wanandoa wengi wajitolee kufanya umisheni, si wa muda mfupi tu, bali kwa wengine kama wito kamili wa maisha. Omba kwamba baadhi ya wanaoitikia watumwe na Bwana wa mavuno kwenye mashamba ya mavuno katika jamii za miji ya ndani ya Marekani ambayo haijafikiwa. Zaidi ya hayo, tuombe kwa bidii kwamba makanisa ya ndani ya majiji yaunganishe juhudi zao, fedha, mipango, na miradi ili kutoa mchango wao wa kipekee na wenye nguvu katika utume wa kimataifa na wa ndani ya nchi. Omba ili Mungu aguse mioyo ya wale wanaosimamia mashirika mengi ya kimishenari, ili kwamba wasipuuze tena rasilimali tajiri za makanisa ya mijini, bali wafanye iwezekane kwa wanafunzi wa mijini kutumwa kupeleka Injili, kufuasa na kupanda makanisa, hasa miongoni mwa makumi na makumi ya jamii ambamo hakuna uwepo wa kiinjili. Zaidi ya yote, tumlilie Mungu mchana na usiku kwa ajili ya kiwango kipya cha msimamo na nidhamu katika maisha na ufuasi wa watu wake. Omba kwa ajili ya imani thabiti lakini yenye moyo mwororo ili kukumbatia makusanyiko madogo na yale yanayoabudia katika kumbi ndogo za maduka ya mijini. Tuwaombee ili Mungu awape ufahamu juu ya vita vya ufalme, aina ya mtazamo thabiti ambao utawawezesha wanafunzi wa mijini kuchukua mtazamo muhimu wa kuvumilia ugumu na kuteseka katika vita vya kiroho kwa niaba ya jamii zao. Tuombe kwa ajili ya viwango vipya vya ujasiri na nguvu, kwa ajili ya mikakati mipya na thabiti

Made with FlippingBook Annual report maker