https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

/ 3 8 9

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

Mungu Wetu Asimame! (muendelezo)

ya kuifikia jamii, kwa ajili ya harakati za maombi ya kumaanisha zaidi na endelevu katika makanisa ya mijini, na mitandao mipya ya uongozi na usaidizi ambayo itaunganisha wanafunzi wa mijini wenye nia njema kuhamasisha rasilimali zao ili kuleta matokeo ya juu zaidi katika miji na majiji yao. Omba kwa bidii kwa Mungu ili aweze kuyapa rasilimali makanisa ya mijini kwa ajili ya kuanzisha huduma mpya za matendo mema, haki, na amani kwa watu wasio na makazi, wanaokandamizwa, yatima, wenye shida ya kiakili, wanaosumbuliwa na VVU na magonjwa mengine ya kuambukiza, kwa wazee, wagonjwa, wafungwa na waliotelekezwa. Omba kwamba Kanisa liweze kujawa na kueneza upendo wa pekee ambao utawavutia waliopotea na kuumba njaa mpya ndani yao kwa ajili ya Yesu, aina ya upendo ambao utatumika kama msingi wa kueleza na kuthibitisha Injili ya Kristo. Omba kwamba Mungu atumie juhudi za kutafuta haki na usawa kama mlango kwa ajili ya malaki ya watu kuupokea wokovu wa Bwana. Usiache kuombea eneo lako kimahususi, na hitaji lake la kuona ishara za Ufalme zikidhihirishwa ndani yake kwa maneno na matendo. Ombea kanisa lako, mchungaji wako, jamii yako, viongozi wa kiraia na wa jiji, majirani zako, wakuu wa shule, maafisa wa sheria, na wengine wote katika uongozi wa jamii yenu. Omba kwa ajili ya kuachiliwa kwa viwango vipya vya ujasiri na uwazi katika kuhubiri, na ishara halisi zaidi za Ufalme katika jamii yako ili Mungu aweze kuwafunulia waliopotea ukuu na ajabu za Bwana Yesu. Jiombee mwenyewe na familia kwa ajili ya upatikanaji mpya ili kuona Ufalme ukienea katika eneo lako la kazi, shuleni kwako, ujirani wako, familia yako, na katika maisha yako. Mungu atatujibu ikiwa tu tutamwomba kwa imani na kujisalimisha kwa kumaanisha kwa mapenzi yake (Mt. 6:6; Yoh. 15:16). Wazo zima la Mungu Wetu Asimame! lilianza kwa imani kubwa kwamba majiji ya Marekani hayawezi kuvunwa bila uingiliaji kati wa moja kwa moja na upaji wa Bwana. Ugumu wa uwanja huu unaweka wazi na bayana ukweli wa hoja ya mtunga zaburi katika Zaburi 127:1: “Bwana asipoijenga nyumba Waijengao wafanya kazi bure. Bwana asipoulinda mji Yeye aulindaye akesha bure.” Vuguvugu hili linaamini kwamba juhudi zozote za kuvuna mamilioni ya watu ambao hawajafikiwa katika miji ya Marekani zitakuwa bure ikiwa Mungu hatatembelea miji hiyo. Tunaamini zaidi kwamba kujiliwa huku kutatokea tu ikiwa wanaume na wanawake watauwa watamlingana Mungu katika maombi na maombezi kwa ajili ya majiji. Ni mpenyo wa nguvu za Mungu pekee utakaoweza kubadilisha miji yetu. Katika Miji ya Marekani

Made with FlippingBook Annual report maker