https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
3 9 0 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
Mungu Wetu Asimame! (muendelezo)
Ingawa ujenzi wa jiji bila shaka ndio ubunifu mkubwa zaidi wa wanadamu katika ustaarabu, hauna chochote cha kujitukuza ndani yake. Jiji kubwa la kisasa ni ngome ya ukosefu wa haki, kutomcha Mungu, na ukosefu wa maadili. Kwa kweli, haiwezekani kuifikiria Marekani bila miji yake mikuu na yenye ushawishi mkubwa – New York, Washington D.C., Los Angeles, Philadelphia, Chicago, Houston, Miami, San Francisco, Boston, Portland, Atlanta, Denver, St. Louis, Dallas, Seattle, San Antonio, n.k. Majiji haya makubwa ni vituo vikubwa zaidi vya utamaduni, elimu, sanaa, tiba, sheria, serikali, siasa, biashara, viwanda, burudani na mamlaka. Hata hivyo pia yanawakilisha baadhi ya sehemu zenye watu waliokata tamaa zaidi duniani; miji yetu imejaa mamilioni ya watu ambao maisha yao yamejawa na anasa tupu, ukosefu mkubwa wa haki, na matukio ya kutisha. Bila shaka, viwango vya giza, umaskini, na kuvunjika moyo katika miji na majiji ya Marekani viko juu sana. Cha kusikitisha ni kwamba, makusanyiko mengi ya kiinjili na madhehebu ya Kikristo yameiacha miji, wakikimbilia mazingira tulivu ya vitongoji, huku wakihamisha pamoja nao Vyuo vyao vya Biblia, seminari, nyumba za uchapishaji za Kikristo, na mashirika ya Kikristo. Waamini wameiacha miji kwa idadi kubwa, na kuwaacha wale wasiomjua Kristo waendelee na hila zao na uonevu. Wakiwa wameridhika kuudunisha Ukristo katika aina yao ya dini finyu, waumini wa Kiinjili wengi wamepunguza wigo wa Tamthilia ya Ulimwengu; wamepunguza wito mkuu wa imani iokoayo katika Kristo kuwa maadili ya familia, ari kubwa ya kizalendo na uhafidhina wa kisiasa. Pasipo hata kusumbuliwa katika dhamiri zao, Wakristo wengi wamegeuzia kisogo kilio cha watu wengi wanaokufa katika majiji. Kwa Kanisa lililoitwa kuwa kama Mwalimu wetu, hili halikubaliki kabisa! Vipengele viwili vya mwisho vya tamasha la maombi la Mungu Wetu Asimame! , yaani Uthibitisho na Ukiri mtawalia, vinatoa fursa ya kutoa shuhuda na maombi ya mwisho ambayo yanathibitisha ukweli wa Mungu juu yake mwenyewe na nia yake ya kuvuna miji na majiji. Ingawa tunathibitisha uwepo wa ukandamizaji wa kikatili na uovu unaoendelea katika miji na majiji, kadhalika tunathibitisha tumaini la wokovu wa miji na majiji, kama ilivyokuwa kwa Ninawi katika kitabu cha Yona, jiji kuu la ukatili la Ashuru, ambalo Mungu alilisamehe. Katika kusamehe kwake kosa lao na kughairi kwake hukumu juu ya jiji hilo lenye giza, tunaona upendo mwingi wa Mungu Uthibitisho na Ukiri
Made with FlippingBook Annual report maker