https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
/ 3 9 1
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
Mungu Wetu Asimame! (muendelezo)
kwa wanadamu waliopotea na kuasi, na nia yake ya kughairi kulihukumu hata jiji lenye uovu zaidi ikiwa wakaazi wake watajinyenyekeza tu mbele zake. Ikiwa Mungu aliiokoa Ninawi ya wakati wa Biblia iliyojaa maelfu, bila shaka tunaweza kuthibitisha kwamba Mungu huyo huyo anaweza kuikomboa New York iliyojaa makumi ya mamilioni ya watu, au Mexico City iliyojaa dazeni za mamilioni! Ulinganisho huo ni wa kibiblia na unashawishi; Mungu Mwenyezi hujibu kilio cha waliopondeka mioyo, waliojutia dhambi na makosa yao na kutubu (Zab. 34:18). Wakati wa kipindi cha Uthibitisho , tunathibitisha kwa Mungu kwa njia ya maombi na kwa kila mmoja wetu kupitia shuhuda za yale ambayo Bwana amesema nasi wakati wetu wa kumtafuta na kumsihi. Tunathibitisha upendo wa milele wa Mungu ambaye alimtuma Mwana wake wa pekee kwa ajili ya ukombozi wetu ( Yoh. 3:16 ), na tunakumbushana kuhusu hatua ya kihistoria ya Mungu kuitikia wakati watu wake, walioitwa kwa jina lake, walipojinyenyekeza, kuomba, na kuutafuta uso wake; na kutubu na kuacha njia zao mbaya za kujishughulisha na mambo yao tu, kujifurahisha wenyewe, na kujitegemea (2 Nya. 7:14). Mungu hufanya kazi kwa kuwaitikia watu wake wanaomlilia katika dhiki zao, kwa kupondeka mioyo, na katika uhitaji wao mbele zake (Kum. 26:5-10). Tunamaliza kipindi chetu cha Uthibitisho kwa maombi ya mwisho ambapo Tunakiri ukweli na ukuu wa Mungu. Tunafanya agano pamoja kumngoja Bwana, kutazamia kuja kwake, kwake yeye pekee awezaye kuimarisha mioyo yetu (Zab. 27:14). Ingawa tunaweza kuchoka katika maombi yetu, tunahakikishiwa kwamba tutashinda pamoja na Mungu, kwa kuwa tunaomba kulingana na mapenzi na nia yake (Isa. 40:28-31). Hatutakuwa na shaka au kukata tamaa au kuvunjika moyo (Yakobo 1.5; Gal. 6:9). Tukianza kufanya maombezi, tunaweza kushawishika kulegea, lakini, kama yule mjane aliyemsumbua kadhi hadi akamjibu, tunakumbushana kwamba ni lazima tuendelee kumwomba Mungu atutendee mpaka ajibu (Luka 18:1-8). Mioyo yetu imedhamiria, nasi tumeazimia, kama mzee wa ukoo Yakobo, kushindana mweleka na Mungu, kumsihi, kumshika na kutomwacha aende zake mpaka atubariki (Mwa. 32:24-32). Kama Yehoshafati, hatuna nguvu dhidi ya watawala wa giza hili la sasa na majeshi ya kiroho yaliyokusanyika kuharibu miji ya Marekani, wala hatujui la kufanya, lakini macho yetu yanamtazama Bwana (2 Nya. 20:12). Tunaamini kwamba siku moja Mungu atampa Mwana wake miji ya ulimwengu huu (pamoja na miji ya Marekani!), ambayo ni sehemu moja tu muhimu ya urithi ambao Baba amependezwa kumpa Bwana Aliyefufuka (Zab. 2:8). Tukijua kwamba Bwana wetu Yesu lazima atawale mpaka adui zake wote wawekwe chini ya miguu
Made with FlippingBook Annual report maker