https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

3 9 2 /

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

Mungu Wetu Asimame! (muendelezo)

yake (1 Kor. 15:24-28), hatutakuwa na shaka na nia yake wala hatutakosa subira kwa habari ya wakati wa majibu yake. Mungu atatujibu, kwa wakati wake na kwa njia yake mwenyewe. Tunapoondoka kwenye mkusanyiko wetu ili kutawanyika tena katika maeneo yetu mahususi ya ushawishi na mahusiano, tunakubali utegemezi wetu kwake, kwamba kipindi chetu cha maombi kimekuwa cha nusu saa, asubuhi nzima, au siku nzima na wiki za kufunga na maombi, tunajua kwamba ahadi ya Bwana ni ya hakika. Isaya 55:6-11 - Mtafuteni Bwana, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu; 7 Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie Bwana, Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa. 8 Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema Bwana. 9 Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu. 10 Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula; 11 ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma. Kweli, Neno la Bwana haliwezi kumrudia bila matunda au tupu. Makusudi ya Mungu wetu, Mungu huyu mkuu, yatasimama (Isa.40:8)! Hitimisho: Jibu kwa Unyenyekevu kwa Wito wa Dhati wa Maombi Endelevu kwa ajili ya Majiji Rafiki mpendwa, ebu nikuulize swali: Je, unachukulia nini kuwa hitaji muhimu la sasa kwa habari ya miji ya Marekani? Akilini mwangu, sio kuingizwa kwa biashara na pesa zaidi, wala si mkusanyiko mpya wa wanasiasa bora, mipango bora ya kukomesha uhalifu mijini, semina za kupanga uzazi, wala programu za chakula. Hitaji kuu la majiji ni Bwana kufanya uwepo wake ujulikane ndani yake. Jambo la kuamua ambalo litasababisha mabadiliko ya miji ya Marekani ni kutembelewa na Mungu, kumiminwa mara kwa mara kwa Roho Mtakatifu katikati ya watu wake katika jiji. Nyakati hizo za kutembelewa na uwepo na nguvu za Mungu zitaleta mapinduzi katika jamii hizi; kutembelewa na Mungu kutasababisha aina mbalimbali za uponyaji, huduma kwa

Made with FlippingBook Annual report maker