https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
/ 3 9 3
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
Mungu Wetu Asimame! (muendelezo)
wahitaji, na haki kwa kiasi ambacho hakuna mtu yeyote angeweza kuelezea, hata yule mtu wa mrengo wa kisiasa wa kiliberali au mtu mkaidi asiyeamini katika Mungu. Zaburi 68 ni ushuhuda wa kile kinachoweza kutokea wakati Bwana anaposhuka, kwa maneno mengine, anapoinuka na kuwatawanya adui zake, na kuacha katika kuinuka kwake baraka za upendo wake mkuu wa moyoni kwa ajili ya wanadamu: 1 Mungu huondoka, adui zake wakatawanyika, Nao wamchukiao huukimbia uso wake. 2 Kama moshi upeperushwavyo, Ndivyo uwapeperushavyo wao; Kama nta iyeyukavyo mbele ya moto, Ndivyo waovu wapoteavyo usoni pa Mungu. 3 Bali wenye haki hufurahi, Na kuushangilia uso wa Mungu, Naam, hupiga kelele kwa furaha. 4 Mwimbieni Mungu, lisifuni jina lake, Mtengenezeeni njia ya barabara, Apitaye majangwani kama mpanda farasi; Jina lake ni YAHU; shangilieni mbele zake. 5 Baba wa yatima na mwamuzi wa wajane, Mungu katika kao lake takatifu. 6 Mungu huwakalisha wapweke nyumbani; Huwatoa wafungwa wakae hali ya kufanikiwa; Bali wakaidi hukaa katika nchi kavu. 7 Ee Mungu, ulipotoka mbele ya watu wako, Ulipopita nyikani, 8 Nchi ilitetemeka Naam, mbingu zilidondoka usoni pa Mungu; Hata Sinai usoni pa Mungu; Mungu wa Israeli. 9 Ee Mungu, ulinyesha mvua ya neema; Urithi wako ulipochoka uliutia nguvu. 10 Kabila yako ilifanya kao lake huko; Ee Mungu, kwa wema wako uliwaruzuku walioonewa. ~ Zaburi 68:1-10
Mungu Wetu Asimame! katikati ya watu wake! Mungu Wetu Asimame! katikati ya uchafu na uozo wa mijini! Mungu Wetu Asimame! katika viti vya mamlaka na ushawishi!
Made with FlippingBook Annual report maker